WHO: Covid-19 ni janga baya zaidi la afya linaloikabili dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62459-who_covid_19_ni_janga_baya_zaidi_la_afya_linaloikabili_dunia
Maambukizi mapya ya virusi vya corona yaliyopelekea watu zaidi ya milioni 16 kuathiriwa na virusi hivyo ni janga baya zaidi la kiafya duniani kuwahi kulikumba Shirika la Afya Duniani (WHO).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2020 00:13 UTC
  • WHO: Covid-19 ni janga baya zaidi la afya linaloikabili dunia

Maambukizi mapya ya virusi vya corona yaliyopelekea watu zaidi ya milioni 16 kuathiriwa na virusi hivyo ni janga baya zaidi la kiafya duniani kuwahi kulikumba Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hayo yalisema jana Jumatatu na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dakta Tedros Adhanom Gebreyesus mbele ya waandishi wa habari huko Geneva Uswisi. Aliongeza kwamba, kuchukua hatua kali za kiafya yaani kuanzia kuvaa barakoa hadi kujiepusha na misongamano ya watu ndiko kutakakoiwezesha dunia kudhibiti maradhi ya Covid-19.

Adhanom amesema kuwa kesi za mamabukizi ya corona zinapunga pale ambako hatua zote hizi zinachukuliwa na kinyyume chake huongezeka pale hatua hizo zinapopuuzwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameongeza kuwa, ongezeko la kesi mpya za maambukizi ya corona katika nchi mbalimbali zikiwemo zile zinazodhani kuwa zimeshaudhibiti ugonjwa wa Covid-19 zinatishia ulimwengu huku idadi ya vifo ikikaribia 650,000.

Wakati huo huuo Mkuu wa Programu za Dharura wa WHO Dakta Mike Ryan amesema kuwa, kuna haja kwa nchi mbalimbali kuchukua hatua kali kama zile za kuzuia mikusanyiko ya watu.

Maafisa wa WHO wamesema kuwa, kipaumbele chao ni kuokoa maisha ya watu na ikiwezekana kukomesha kabisa vifo na kupunguza idadi ya vifo hadi kiwango cha chini. 

Dakta Mike Ryan, Mkuu wa Programu za Dharura wa WHO