Russia yasisitiza udharura wa kustawisha uhusiano na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64177-russia_yasisitiza_udharura_wa_kustawisha_uhusiano_na_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa nchi hiyo itaendeleza uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran licha ya vitisho vya Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 22, 2020 23:27 UTC
  • Russia yasisitiza udharura wa kustawisha uhusiano na Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa nchi hiyo itaendeleza uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran licha ya vitisho vya Marekani.

Maria Zakharova amesema kuwa Marekani imetangaza kwamba lengo la Washington ni kuzizuia nchi nyingine kushirikiana na Iran lakini Russia, kwa upande wake, itaendelea kushirikiana na Iran katika nyanja za kiufundi na kijeshi.   

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa Moscow na Tehran zinashirikaina pia katika nyuga za kimataifa kama vile katika mazungumzo ya Astana ya kutatua hitilafu na kadhia ya Syria.  

Bi Zakharova amesema kuwa suala la kupambana na ugonjwa wa Covid-19 pia linapewa kipaumbele na viongozi wa Iran na Russia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa, Iran na Russia zitaendelea kushirikiana kwa ajili ya maslahi ya pande mbili  na kustafidi na suhula na uwezo mkubwa wa nchi hizo. 

Maambukizi ya corona 

Marekani imeiwekea Iran mashinikizo ya kila upande baada ya kujitoa kenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA tarehe 8 mwezi Mei mwaka 2018. Washington pia inadai kuwa lengo la mashinikizo yake ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya Iran ni kufikia mapatano mapya na Tehran.