Viongozi wa Marekani waendeleza misimamo yao ya kiuadui dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65204-viongozi_wa_marekani_waendeleza_misimamo_yao_ya_kiuadui_dhidi_ya_iran
Ikiwa ni katika kudumisha misimamo ya uhasama ya viongozi wa White House dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mjumbe maalumu wa serikali ya Marekani anayeshughulikia masuala ya Iran ameunga mkono vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran.
(last modified 2026-05-13T14:18:38+00:00 )
Dec 15, 2020 04:38 UTC
  • Viongozi wa Marekani waendeleza misimamo yao ya kiuadui dhidi ya Iran

Ikiwa ni katika kudumisha misimamo ya uhasama ya viongozi wa White House dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mjumbe maalumu wa serikali ya Marekani anayeshughulikia masuala ya Iran ameunga mkono vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran.

Akizungumza hivi karibuni na gazeti la Kizayuni la Times of Israel  mjumbe huyo maalumu Elliott Abrams,  amesema mapatano ya nyuklia ya JCPOA yalikuwa na kasoro nyingi na kwamba msimamo wa Washington na wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, ni mmoja kuhusu suala hilo.

Abrams ameendelea kusema kuwa yeye na viongozi wengine wote wa serikali ya Rais Dond Trump wamekutana na kuzungumza na maafisa wa timu ya mpito ya Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani kuhusu mapatano ya JCPOA.

Huku akikariri misimamo ya viongozi wa Marekani iliyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abrahams amesema kuwa serikali ya Trump ilipasa kuanza kutekeleza mapema zaidi siasa za 'mashinikizo ya juu kabisa' dhidi ya Iran.

Mara tu baada ya kujitoa katika mapatano ya JCPOA Mei 2018 serikali ya Marekani ilirejesha vikwazo dhidi ya Iran na kuanza kutekeleza siasa za kichochezi dhidi yake.

Elliott Abrams

Trump alikuwa ametoa ahadi kwamba kwa kutekeleza siasa hizo za mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Iran, angewalazimisha viongozi wa Tehran wasalimu amri na kumuomba waketi naye kwenye meza ya mazungumzo, ili eti kuweza kufikia mazungumzo mazuri zaidi.

Baada ya kupita miaka minne si tu kwamba ndoto yake hiyo haijatimia bali amefedheheka kwa kufukuzwa madarakani na Wamarekani huku ukosoaji mkubwa wa makundi tofauti ya Marekani ukiwa unamwandama.

Wakosoaji wake wanamlaumu kwa kutokuwa na stratijia maalumu kuhusu Iran, kuzidisha mivutano isiyo na maana na nchi hii na vilevile kuwatenga washirika wake barani Ulaya.