Jul 13, 2021 02:34 UTC
  • Mbunge Mmarekani akiri kushindwa vibaya nchi yake huko Afghanistan

Mbunge mmoja wa chama cha Republican cha Marekani amekiri kuwa Washington imeshindwa vibaya nchni Afghanistan na ametaka wanajeshi wa Marekani warudishwe haraka nchini humo.

Mbunge Adam Kinzinger amekiri kwamba operesheni za wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan zimefeli vibaya. Amesema: "Huku ni kufeli vibaya sana, mimi kwa hakika nimesikitishwa mno na jambo hilo."

Akitangaza upinzani wake kuhusu uamuzi wa Marekani wa kukimbiza wanajeshi wake Afghanistan amesema, mimi najifakharisha na operesheni za miaka 20 za wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan na kwa yakini ninaamini kwamba kuna wajibu wanajeshi hao waendelee kubakia muda mrefu zaidi nchini humo.

Adam Kinzinger

 

 

Mwezi Februari 2020, Washington na kundi la Taliban zilifikia makubaliano ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan na sasa hivi mchakato wa kutoka wanajeshi hao na waitifaki wao, umeanza. 

Kukimbia kwa fedheha wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kunafanyika katika hali ambayo karibu miaka 20 ya kuweko wanajeshi hao vamizi huko Afghanistan hakukuwaletea wananchi madhulumu wa nchi hiyo ya Waislamu zaidi ya matatizo, machafuko, njaa, umaskini wa kupindukia, ukosefu mkubwa wa usalama, kuharibiwa miundombinu na ongezeko kubwa la uzalishaji na utumiaji wa madawa haramu ya kulevya. 

Mara chungu nzima wakuu wa Afghanistan wamekuwa wakishinikiza kutoka wanajeshi wote wa kigeni nchini humo, na wanasisitiza kwamba Waafghani wenyewe wanao uwezo wa kujilinda na kujiendeshea mambo yao.

Tags