Chomsky: Vita vya Marekani dhidi ya 'ugaidi' vimesababisha uharibifu duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i74476-chomsky_vita_vya_marekani_dhidi_ya_'ugaidi'_vimesababisha_uharibifu_duniani
Mwanafalsafa na mwanahistoria mashuhuri wa Marekani amesema vita vilivyoanzishwa na Washington miaka 20 iliyopita kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi vimesababisha uharibifu katika sehemu kubwa ya dunia.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Sep 09, 2021 22:17 UTC
  • Chomsky: Vita vya Marekani dhidi ya 'ugaidi' vimesababisha uharibifu duniani

Mwanafalsafa na mwanahistoria mashuhuri wa Marekani amesema vita vilivyoanzishwa na Washington miaka 20 iliyopita kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi vimesababisha uharibifu katika sehemu kubwa ya dunia.

Noam Chomsky aliyekuwa akizungumza kwa mnasaba wa kutimia miaka 20 tangu baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huko Marekani, amesema kuwa, uharibifu uliofanywa katika sehemu kubwa ya Asia ya Kati na Magharibi mwa Asia kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi haujazidisha chochote katika nguvu na uwezo wa Marekani.

Chomsky amesema: "Wakati Marekani iliposhambulia na kuivamia Afghanistan ugaidi ulikuwa katika sehemu moja tu ya nchi hiyo, lakini sasa vituo vya ugaidi vimeenea katika maeneo yote ya dunia." 

Wapiganaji wa kundi la Daesh huko Iraq na Syria

Noam Chomsky amesema, uchunguzi wa maoni wa kimataifa unaonesha kuwa, Marekani ndio tishio kubwa zaidi la amani ya kimataifa na kuongeza kuwa: Mashambulizi dhidi ya Afghanistan yalikiuka sheria za kimataifa na hayawezi kuhalalishwa kwa kisingizio chochote cha maana. 

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, mwanahistoria huyo mashuhuri amesema nguvu ya Marekani imeporomoka kwa kiwango kikubwa na kwamba jambo hilo lilionekana wazi hata kabla ya Donald Trump kutoa pigo kubwa kwa hadhi ya nchi hiyo. 

Msomi na mchambuzi huyo mkubwa wa Marekani pia amekosoa mapatano yaliyofikiwa baina yaDoland Trump na kundi la Taliban Februari mwaka jana na kusemja: Katika mapamtano hayo ya kuondoka Afghanistan, Trump hakushauriana hata na serikali rasmi ya Afghanistan bali aliilazimisha Kabul kuwaachia huru wapiganaji elfu tano wa kundi la Taliban.