Trump: Marekani inaelekea kuwa shimo la maji taka kutokana na wahamiaji
-
Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ameashiria wimbi kubwa la wahajiri wanaomiminika nchini humo na kusema: Marekani inaelekea kuwa shimo la maji taka.
Taarifa iliyotolewa na Donald Trump imesema kuwa, wimbi la wahajiri wanaoingia Marekani yumkini likawa mgogoro mkubwa zaidi unaoikabili nchi hiyo.
Trump ameongeza kuwa, idadi kubwa ya mamiilioni ya wageni wanaendelea kumiminika kinyume cha sheria nchini Marekani.
Rais huyo wa zamani wa Marekani amedai kuwa, wahajiri hao raia wa kigeni ndio wanaounda sehemu kubwa ya makatili, wauaji, walanguzi wa dawa za kulevya na wahalifu wa aina mbalimbali nchini Marekani.
Katika siku za karibuni Trump amekuwa akimkosoa sana Rais Joe Biden aliyechuana naye katika uchaguzi uliopita wa rais kutokana na kufeli kwa serikali yake katika masuala mengi na kusema, Marekani inastahiki kiongozi bora zaidi kuliko Biden.