Asilimia 70 ya Wademocrat hawataki Trump agombee urais mwaka 2024
https://parstoday.ir/sw/news/world-i75100-asilimia_70_ya_wademocrat_hawataki_trump_agombee_urais_mwaka_2024
Asilimia 70 ya Wademocrat nchini Marekani wanapinga jaribio la aina yoyote la rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump kugombea katika uchaguzi wa rais mwaka 2024.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 27, 2021 01:02 UTC
  • Asilimia 70 ya Wademocrat hawataki Trump agombee urais mwaka 2024

Asilimia 70 ya Wademocrat nchini Marekani wanapinga jaribio la aina yoyote la rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump kugombea katika uchaguzi wa rais mwaka 2024.

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Echelon Insights yanaonesha kuwa, ni asilimia 30 ya wanachama wa chama cha Democratic wanaotaka Trump agombee kiti hicho bila ya mpinzani ndani ya chama hicho. 

Katika mahojiano yake ya karibuni, rais huyo wa zamani wa Marekani aliiambia televisheni ya Fox News kwamba, ana nia ya kugombea tena katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka 2024. 

Hii ni licha ya kuwa, Donald Trump ni rais pekee katika historia ya Marekani ambaye ameitwa na kusailiwa bungeni mara mbili kwa kutumia vibaya madaraka yake, kutatiza kazi za Kongresi na kuchochea wafuasi wake kushambulia jengo la Capitol Hill hapo taree 6 Januari mwaka 2020.