Emmanuel Macron ashutumiwa kwa kujaribu 'kumsafisha' Mohammed bin Salman
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa mkutano wa Rais Emmanuel Macron na Ufaransa na mriti wa ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman jana Jumamosi huko Riyadh yakisisitiza kuwa mkutano huo una lengo la kumsafisha mrithi huo wa ufalme wa Saudia aliyeamuru kuuawa kigaidi mwandishi habari jamal Khashoggi.
Mazungumzo na mkutano Macron na Bin Salman ni wa kwanza wa kiongozi wa nchi ya Magharibi na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia tangu serikali ya Riyadh ilipotekeleza mauaji ya kigaidi dhidi ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mjini Istanbul mwaka 2018.
Kwa kipindi chote cha miaka mitatu iliyopita tangu baada ya mauaji hayo, wakuu wa nchi za Magharibi wameepuka mikutano na mazungumzo ya moja kwa moja na mrithi huyo wa ufalme Saudia ambaye anametajwa kuwa ndiye aliyetoa amri ya kuuawa kigaidi mwandishi habari na mkosoaji wa utawala wa kifalme wa Saudia, Jamal Khashoggi.
Hatua hiyo ya Macron inakuja chini ya mwaka mmoja baada ya mashirika ya kijasusi ya Marekani kutoa ripoti iliyosema, yanaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya Khashoggi.
Agnès Callamard, raia wa Ufaransa ambaye ni Katibu Mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International amesema: "Hakuna kinachoweza kutetea hatua ya Macron ya kutaka kuhalali mtawala anayeua waandishi wa habari, kutishia wanaharakati, kuwafunga wanawake watetezi wa haki za binadamu, kuchinja raia wa Yemeni na kuidanganya jamii iya ya kimataifa." Callamard ameongeza kuwa, Macron anajishushia hadhi yake yeye na nchi yake anaposhirikiana na Mohammad bin Salman."
Bin Salman ameshtakiwa kwa makosa ya kumteka nyara na kumuua Jamal Khashoggi. Makosa mengine ni kumtesa na kumuua kinyama na kikatili mno Jamal Khashoggi, unyama ambao umeishitua dunia nzima.
Khashoggi aliuawa kikatili katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki na mwili wake kukatwa vipande vipande.