Lavrov: Video za "Bucha" ni kisingizio cha kuharibu mazungumzo yanayoendelea Istanbul
-
Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amelilaumu jeshi la Ukraine na idara za usalama za nchi hiyo kwa kubuni mkanda wa video eti ya mauaji ya mji wa Bucha na kuongeza: "Hiki ni kisingizio cha kuvuruga mazungumzo yanayoendelea Istanbul."
Sergei Lavrov amesema katika video iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia kuhusu Ukraine kwamba: "Katika siku chache zilizopita, mashine za propaganda za nchi za Magharibi na Ukraine zimekuwa zikichochea mvutano kuhusu video zilizochukuliwa na jeshi la Ukraine na idara ya usalama za nchi hiyo kwenye eneo la Bucha katika mkoa wa Kiev.
Akiuliza swala kwamba, ni nini madhumuni ya uchochezi huu wa wazi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rusia amejibu kwa kusma: "Suala hili ni kisingizio cha kuharibu mazungumzo ya sasa wakati mwanga, ingawa mdogo, unaonekana mwishoni mwa njia."
Sergei Lavrov amesema: "Katika mazungumzo ya Istanbul tarehe 29 Machi 2022, wawakilishi wa Ukraine, kwa mara ya kwanza waliwasiliana na wajumbe wetu, na kutoa maoni yao kwa maandishi juu ya makubaliano ya hali ya Ukraine na dhamana ya usalama."
Itakumbukwa kuwa picha za maiti zilizokuwa zimezagaa katika barabara za eneo la Bucha huko Ukraine zimeiacha dunia bumbuazi huku vyombo vya Magharibi vikitumia suala hilo kuchochea propaganda chafu dhidi ya Rusia. Picha hizo zilisambazwa kote duniani sambamba na tangazo lililotolewa na serikali ya Ukraine mnamo Aprili 3 kwamba maeneo yote ya mji mkuu yalikuwa yamekombolewa kutoka kwenye udhibiti wa Russia.
Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilichapisha kwa wingi picha za mji wa Bucha karibu na Kiev, vikidai kuwa vikosi vya jeshi la Russia vimewafyatulia risasi raia vilipokuwa vikiondoka katika mji mkuu wa Ukraine.
Hata hivyo Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, ilisema Jumanne iliyopita kwamba shutuma za nchi za Magharibi kwamba vikosi vya jeshi la Russia vilifanya uhalifu wa kivita kwa kuwaua raia huko Bucha, ni za uzushi unaolenga kuchafua jina la jeshi la nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Rusia pia imesema katika taarifa kwamba: "Vitengo vyote vya jeshi la Russia viliondoka kabisa Bucha mnamo Machi 30, siku moja baada ya mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Russia na Ukraine nchini Uturuki.