Wasiwasi Waongezeka Marekani kutokana na kushadidi visa vya uhalifu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i82270-wasiwasi_waongezeka_marekani_kutokana_na_kushadidi_visa_vya_uhalifu
Wasiwasi wa watu wa Marekani kuhusu uhalifu wa kutumia silaha za moto umefikia kiwango cha juu zaidi tangu 2016.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 08, 2022 03:48 UTC
  • Wasiwasi Waongezeka Marekani kutokana na kushadidi visa vya uhalifu

Wasiwasi wa watu wa Marekani kuhusu uhalifu wa kutumia silaha za moto umefikia kiwango cha juu zaidi tangu 2016.

Ni kutokana na na wimbi la ghasia, utekaji nyara na mashambulizi ya kutumia silaha lililoshika kasi nchini Marekani.

Maelfu ya raia wa Marekani huuawa au kujeruhiwa kila mwaka katika ufyatuaji risasi wa kiholela na katika maneneo ya umma.

Ripoti rasmi zinaonesha kuwa, kuna takriban bunduki milioni 270 hadi 300 nchini Marekani; suala ambalo lina maana kwamba, kuna karibu bunduki moja kwa kila mtu katika nchi hiyo.

Uhuru wa kubeba silaha nchini Marekani unasababisha vurugu na ukatili wa kila siku za nchini humo kakini ushawishi wa lobi za makampuni ya kuzalisha na kuuza silaha una nguvu kubwa kiasi kwamba, Bunge la Marekani limeshindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia ubebaji wa silaha.

Kura ya maoni ya Gallup iliyofanywa kuanzia Machi Mosi hadi 18 ilionesha kuwa, asilimia 88 ya Wamarekani wameeleza wasiwasi wao kuhusu ongezeko la uhalifu nchini humo.

Marekani ina kiwango kikubwa zaidi cha uhalifu wa ufyatuaji risasi duniani, huku wastani wa zaidi ya watu 100 wakiuawa kila siku kwa kufyatuliwa risasi.