Nchi za Afrika zaiunga mkono China katika mzozo na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i8395-nchi_za_afrika_zaiunga_mkono_china_katika_mzozo_na_marekani
Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Erastus Mwencha ameunga mkono msimamo wa China katika suala la bahari ya kusini ya China na kutoa wito kwa nchi husika kutoa fursa ya kuanza mazungumzo kwa ajili ya kutatua suala hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2016 10:03 UTC
  • Nchi za Afrika zaiunga mkono China katika mzozo na Marekani

Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Erastus Mwencha ameunga mkono msimamo wa China katika suala la bahari ya kusini ya China na kutoa wito kwa nchi husika kutoa fursa ya kuanza mazungumzo kwa ajili ya kutatua suala hilo.

Akiongea na mwenyekiti wa muda wa ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Bw. Chen Xuefeng, Bw Mwencha amesema, ni muhimu kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.

Nchi hizo zinatakiwa kufuata sheria za kimataifa, na kanuni za mienendo ya pande husika kwenye bahari ya kusini mwa China ili kutatua suala hilo kwa amani na kuongeza uaminifu wa kisiasa.

Nchi kadhaa zimekuwa zikidai umiliki wa eneo hilo utajiri huko kusini mwa bahari ya China ambapo Marekani inaunga mkono nchi zinazozozana na China kuhusu umiliki wa eneo hilo.

Hivi karibuni Marekani ilisema ndege 2 za jeshi la China zimeizuia ndege moja ya kijeshi ya Marekani iliyokuwa katika anga ya bahari ya kusini mwa China. Marekani inadai kuwa tuukio hilo lilitokea katika anga ya kimataifa mnamo tarehe 17 mwezi Mei wakati wanamaji wa Marekani walipokuwa katika eneo hilo.

Hata hivyo, msemaji wa wizara ya masuala ya nchi za kigeni wa China alikana madai yoyote ya kuhatarishwa usalama kutoka kwa ndege hizo za China.

Hali ya wasiwasi imeongezeka katika Bahari ya Kusini ya China ambapo China na Marekani zinatupiana lawama kuhusu hatua zao za kijeshi. China inasisitiza kuwa Marekani inafanya uchokozi katika eneo lisiloihusu.