Waziri wa Ufaransa akiri kuadimika dizeli na petroli mjini Paris
(last modified Thu, 20 Oct 2022 00:44:52 GMT )
Oct 20, 2022 00:44 UTC
  • Waziri wa Ufaransa akiri kuadimika dizeli na petroli mjini Paris

Waziri wa Usafirishaji wa Nishati wa Ufaransa ametangaza kuadimika mafuta ya dizeli ya petroli katika vituo vya mafuta vya mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.

Ikumbukwe kuwa Ufaransa iko mstari wa mbele katika maamuzi ya Umoja wa Ulaya ya kuiwekea vikwazo Russia kwa kisingizio cha mgogoro wa Ukraine. Nchi za Ulaya zinategemea mno nishati ya bei nafuu ya Russia kujiendesha.

Agnès Pannier-Runacher, waziri wa usafirishaji nishati wa Ufaransa ameiambia redio moja ya nchi hiyo kwamba, licha ya kuweko ishara za kuboreka hali ya mambo lakini mji mkuu wa nchi hiyio Paris hivi sasa umekumbwa na upungufu wa dizeli na petroli katika vituo vyake vya mafuta.

Polisi wa Ufaransa wakikandamiza waandamanaji

 

Jambo jingine lililoiweka kwenye hali mbaya Ufaransa katika masuala ya nishati ni mgomo wa sekta za mafuta. Mgomo wa wafanyakazi wa sekta hiyo umeifanya kiwete Ufaransa hivi sasa na kuongeza wizi wa mafuta katika nchi hiyo ya Ulaya Magharibi, kuliko wizi uliokuweko huko nyuma.

Mgomo wa wafanyakazi wa sekta ya mafuta ya Ufaransa umepunguza mno uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa zaidi ya asilimia 60.

Uhaba wa mafuta uliomkumba mkoloni huyo kizee wa Ulaya hivi sasa umepaisha bei ya bidhaa hiyo muhimu kwa zaidi ya euro moja kwa kila lita wakati ongezeko la bidhaa hiyo huwa ni kwa senti kadhaa tu.

Vile vile uhaba wa mafuta nchini Ufaransa umesababisha matatizo kwenye sehemu nyingi muhimu sana katika usafiri wa umma, magari ya shule, taxi, Zima Moto na hata kwa jeshi la polisi.