Jun 22, 2016 04:06 UTC
  •  UNICEF: Hali ya wakimbizi watoto nchini Ujerumani inasikitisha

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limekosoa vikali hali mbaya inayowakabili wakimbizi watoto nchini Ujerumani na kusema kuwa hawapewi huduma zinazofaa za tiba wala elimu.

Ripoti ya UNICEF imesema kuwa, wakimbizi watoto nchini Ujerumani hawapewi huduma ya elimu kwa miezi kadhaa sasa. Imeongeza kuwa vijana wanahitaji usimamizi na ulinzi bora zaidi kutokana na unyanyasaji wanaokumbana nao katika kambi kubwa na kwamba wakimbizi watoto waliopatwa na matatizo ya kinafsi kutokana na mashaka ya vita, wanahitaji huduma maalumu kama za wenzao wa Ujerumani.

Mkuu wa ofisi ya UNICEF nchini Ujerumani, Christian Schneider amesema watoto wote wana haki sawa bila ya kujali wanatoka wapi au ni wa jamii ipi.

Awali Shirika hilo la Watoto la Umoja wa Mataifa lilikuwa tayari limetahadharisha kuwa wakimbizi watoto wanalazimishwa kutenda uhalifu au kujihusisha na ukahaba nchini Ufaransa.

 

 

 

Tags