7
Ureno yaisasambua Ufaransa na kutwaa Kombe la Yuro 2016
Ahlan wasahlan wamarhaba mpenzi msikilizaji wa Radio Tehran na hususan ashiki wa spoti natumai huna neno. Baada ya kupezana kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kupumzishwa kipindi hiki cha Ulimwengu wa Michezo ili kupisha vipindi na mawaidha ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, nakukaribisha kwa moyo mkunjufu nikupashe yaliyojiri viwanjani ndani ya siku saba zilizopita. Nakusihi tuandamane sote hadi tamati ya kipindi.