Feb 26, 2025 12:43 UTC
  • Ustawi mkubwa wa Iran katika sekta ya Akili Mnemba

Karibuni kujiunga nami katika Makala hii ambayo huangazia baadhi ya matukio muhimu nchini Iran katika uga wa Sayansi, Tiba na Teknolojia.

@@@

Akili Mnemba, mojawapo ya nyanja zinazokua kwa kasi zaidi za teknolojia ambayo inabadilisha kwa msingi vipengele vingi vya maisha ya leo, imepiga hatua kubwa nchini Iran, nchi yenye fursa na changamoto za kipekee.

Idadi ya startups zinazofanya kazi katika uchambuzi wa data, kujifunza kwa mashine, na maono ya kompyuta inaongezeka nchini Iran ambako wanatoa huduma mbalimbali kwa wateja kwa kutumia ubunifu wa msingi wa akili mnemba.

Baadhi ya startups hizi zimefanikiwa kuvutia uwekezaji wa ndani na wa kimataifa na zinaendelea kukuza na kupanua shughuli zao polepole.

Moja ya sifa kuu za mfumo wa ikolojia ya Akili Mnemba nchini Iran ni ushirikiano unaoongezeka kati ya vyuo vikuu na sekta ya viwanda. Ushirikiano huu husaidia kampuni mpya na startups kunufaika na maarifa na utafiti wa kisayansi na kutoa bidhaa na huduma mpya kwa kutumia Akili Mnemba.

Ukombozi wa maarifa ya kitaaluma unaonekana kwa kiasi kikubwa kama mfano wa maendeleo ya kiuchumi, hasa kwa kuboresha uwezo na utendaji wa kiuchumi wa maeneo.

Uingiliano kati ya sayansi na viwanda sio tu husaidia kuharakisha maendeleo ya akili mnemba nchini Iran, lakini pia husababisha kuongezeka kwa ufanisi na ushindani wa kampuni hizi katika masoko ya ndani na nje.

Maendeleo ya Iran ya mfululizo wa roboti za humanoid za Surena ni mafanikio makubwa ya nchi katika uwanja wa roboti na akili mnemba. Ikiwa imechambuliwa na Taasisi ya Wahandisi wa Umeme na Elektroniki (IEEE), roboti ya humanoid inayojulikana kwa jina la Jenerali wa Parthian Surena, inachukuliwa kati ya roboti maarufu duniani.

Surena kizazi cha nne, ilichoonyeshwa mwaka 2019, inaweza kutembea kwenye eneo lisilo sawa na kushika vitu kwa udhibiti wa nguvu.

@@@

Mafanikio mengine tunayoweza kuyataja ni ya Balad. Hii ni aplikesheni ya ramani uongozaji inayoshabihiana na GPS. Aplikesheni ya Balad ina uwezo mkubwa wa kupima na kutambua kwa makini kila mahali kwa kutumia Akili Mnembe. Hivi asa aplikesheni hii  imepakuliwa na mamilioni ya watumiaji wa simu za mkononi.

Wazo la kuunda huduma hii ya ramani ya ndani inayotumia teknolojia ya utambuzi wa sauti lilianzishwa baada ya Google Maps kuacha kufanya kazi nchini Iran kutokana na vikwazo vya Marekani.

Programu hiyo husaidia watumiaji kupata njia bora kwa safari ndani na nje ya mji, pamoja na kuchagua mahali bora kwa burudani, utalii, na huduma.

Jarida la Nature linalofuatilia ushirikiano wa makala za kisayansi zenye ubora wa juu limeiweka Iran kama ya 13 duniani katika uga Akili Mnemba kwa mujibu wa machapisho ya utafiti kutoka 2015-2019 – ikiwa imezipiku nchi kubwa kama vile Brazil, Uholanzi na Russia.

Katika Viwango vya Taasisi za Scimago, Iran imeorodheshwa ya 15 duniani na ya kwanza katika Asia Magharibi kwa mujibu wa makala zilizochapishwa zinazohusiana na akili mnemba, baada ya Brazil, huku ikiwa imezipita nchi kama vile Russia na Uturuki.

SCImago ni huduma ya umma inayoorodhesha majarida ya kisayansi na viwango vya uchapishaji kwa nchi, ikichanganya seti tatu tofauti za viashiria kulingana na utendaji wa utafiti, matokeo ya ubunifu na athari za kijamii.

Pia, katika sayansi ya utambuzi au cognitive science , sehemu ya saikolojia, ambayo ni mojawapo ya taaluma zinazohusiana na Akili Mnemba, Iran inashika nafasi ya 36 duniani na ya tatu katika Asia Magharibi.

Katika uhandisi wa umeme na elektroniki, ambayo ni sehemu ya akili mnemba, Iran inashika nafasi ya 15 duniani na ya kwanza katika Asia Magharibi. Chuo Kikuu cha Tehran kinashika nafasi ya 59 kati ya taasisi 100 za juu za utafiti katika uwanja wa Akili Mnemba.

@@@

Sasa tuangazie taarifa za taasisi ya viwando inayojulikana kama CSRankings.  Taasisi huu hutegemea metriki za taasisi za juu za sayansi ya kompyuta duniani kote, na data iliyopatikana kutoka kwa wasifu wa wanasayansi wa kompyuta katika Google Scholar. Kwa mujibu wa kiwango chake cha 2011-2021, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif, Taasisi ya IPM ya Utafiti katika Sayansi za Msingi na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Iran zilikuwa miongoni mwa taasisi 100 za juu barani Asia zinazofanya kazi katika Akili mnemba.

Iran inaendelea kujitokeza kama kiongozi wa kikanda katika nyanja za hali ya juu kama vile akili mnemba, roboti, na nanoteknolojia, ambazo zinapata matumizi mapya katika viwanda mbalimbali.

Hivi karibuni, Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) lilitumia makombora yenye teknolojia ya akili mnemba wakati wa mazoezi ya kijeshi katika Ghuba ya Uajemi.

Jamhuri ya Kiislamu imeweka lengo la kuwa kiongozi wa soko la akili mnemba ifikapo 2032. Ripoti ya Taasisi ya Utafiti wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Iran inaonyesha kuwa Iran itakuwa miongoni mwa nchi 10 bora katika Akili Mnemba duniani ndani ya miaka 10.

Mfumo wa ikolojia wa Akili Mnemba nchini Iran umeimarishwa na roho ya ujasiriamali na ustadi wa kubadilika na kupata suluhisho za kibunifu kwa changamoto zinazotokana na vikwazo visivyo vya haki kwa nchi hiyo.

Kwa kifupi, uwanja wa Akili Mnemba ni fursa ya dhahabu kwa Iran ambayo inahitaji ushirikiano wa kina kati ya serikali, sekta binafsi na vyuo vikuu ili kutumia uwezo wote kwa ajili ya maendeleo yake.

@@@

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa Marekani imeshindwa kuzuia ujenzi wa mtambo wa nyuklia wa Karun katika jiji la Darkhovein, kusini magharibi mwa Iran, akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaendelea kufuatilia shughuli zake za nyuklia kwa amani licha ya njama za maadui.

Mohammad Eslami alisema: "Ulimwengu mzima unajua kuwa Iran inaendelea kupata maarifa ya kujenga mitambo ya nyuklia."

Alitoa matamshi hayo wakati wa hafla iliyofanyika katika eneo la ujenzi wa mtambo wa umeme wa nyuklia wa Karun, uliopo katika Wilaya ya Darkhovein, Kaunti ya Shadegan, mkoa wa Khuzestan.

Aliongeza kuwa: "Ili kufanikisha malengo yetu, hatujali vikwazo na shinikizo kutoka kwa maadui." Pia alibainisha kuwa: "Tutaendelea na njia tuliyojiwekea ili kufanikisha malengo yetu."

Akitaja nafasi ya Iran katika nyanja ya ujuzi wa ujenzi wa mitambo ya nyuklia, Eslami alisema: "Iran imekuwa mhusika mkuu katika maarifa ya kujenga mitambo ya nyuklia duniani, na maadui hawawezi kuvumilia mafanikio haya makubwa."

Akitilia mkazo umuhimu wa ujuzi huu katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tiba na kilimo, Eslami alisisitiza kuwa maadui hawawezi kuizuia Jamhuri ya Kiislamu kufanikisha malengo yake kwa kuwaua wanasayansi wake au kwa kuweka vikwazo na shinikizo la kiuchumi dhidi ya nchi.

Akizungumzia ujenzi wa mtambo wa nyuklia wa Karun wenye uwezo wa megawati 300, mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa operesheni hiyo "inaendelea vizuri."

Akitilia mkazo kwamba Iran inaendelea na shughuli zake za nyuklia kwa amani licha ya mashinikizo, Eslami amesema: "Miaka kumi na miwili iliyopita, Marekani ilijaribu kusimamisha mchakato wa ujenzi wa mtambo wa nyuklia wa Darkhovein lakini imeshindwa."

Kulingana na ripoti, mtambo huo wa nyuklia ni wa aina ya kinu cha nyuklia cha maji yenye shinikizo kubwa (Pressurized Water Reactor - PWR) na una uwezo wa kuzalisha megawati 300 za umeme. Mtambo huu unatarajiwa kujengwa kwenye eneo la takriban hekta 50 karibu na Mto Karun.

@@@

N.....