UN: Sekta ya Afya Gaza imeporomoka kutokana na mashambulizi ya Israel
Karibuni kujiunga nami katika Makala hii ambayo huangazia baadhi ya matukio muhimu nchini Iran katika uga wa Sayansi, Tiba na Teknolojia. Katika Makala hii tutaangazia ripoti za Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kuporomoka katika Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel..
@@@
Amesema "Ulinzi wa hospitali wakati wa vita ni muhimu na lazima uheshimiwe na pande zote, wakati wote,".
Utafiti huo umetolewa siku chache tu baada ya kituo kikuu cha huduma ya afya kilichosalia kufanya kazi kaskazini mwa Gaza, Hospitali ya Kama Adwan, kuzimwa kufanya kazi baada ya uvamizi wa vikosi vya jeshi la Israeli, na kuwaacha wakaazi wa Gaza Kaskazini karibu kukosa kabisa huduma za afya za kutosha.
Wafanyikazi na wagonjwa wamelazimika kutoroka au kuwekwa chini ya ulinzi, na ripoti nyingi za kuteswa na kutendewa vibaya.
Pia mkurugenzi wa hospitali hiyo aliwekwa chini ya ulinzi na hatma yake bado hajulikani aliko.
Ripoti iliyochapishwa Disemba 31 2024 na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imeweka wazi kuwa mtindo wa Israel wa mashambulizi mabaya karibu na dhidi ya hospitali katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi hayo ya utawala katili wa Israel yamesukuma mfumo wa afya kwenye ukingo wa kuelekea kuporomoka kabisa, hali ambayo imekuja na athari mbaya kwa Wapalestina kukosa uwezo wa kupata huduma za afya na matibabu.
Ripoti iliyochapishwa mjini Geneva Uswis ikiorodhesha mashambulizi yaliyofanywa kati ya 12 Oktoba 2023 na 30 Juni 2024, inaelezea wasiwasi mkubwa kuhusu Israeli kufuata na kuheshimu sheria za kimataifa.
Wahudumu wa afya na hospitali wanalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu, mradi hawatendi au hawatumiwi kufanya, nje ya kazi zao za kibinadamu kutenda madhara kwa adui imesema ripoti.
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za binadamu Volker Türk amesema kana kwamba mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu na hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza havitoshi, mahali pa kimbilio kama Hospitali ambapo Wapalestina walipaswa kuhisi kuwa salama sasa pamekuwa pakawa mtego wa kifo.
@@@
Uwezekano wa uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu
Katika kipindi kilichoangaziwa na ripoti hiyo, kulikuwa na mashambulizi yasiyopungua 136 katika hospitali 27 na vituo vingine 12 vya matibabu, yakisababisha hasara kubwa kati ya madaktari, wauguzi, huduma za matabibu na raia wengine, na kusababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni Pamoja na wa miundombinu ya raia.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa, hata katika hali ya kipekee wakati wahudumu wa afya, magari ya kubebea wagonjwa, na hospitali wanapopoteza ulinzi wao kwa sababu wanatimiza vigezo vikali vya kuchukuliwa kuwa ni walengwa kijeshi, shambulio lolote dhidi yao bado lazima lizingatie kanuni za msingi za kutofautisha, uwiano na tahadhari katika mashambulizi.
Ripoti imesisitiza kuwa Kukosa kuheshimu mojawapo ya kanuni hizi kunajumuisha uvunjaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
Na kuongeza kuwa Kuelekeza mashambulizi kwa makusudi dhidi ya hospitali na mahali ambapo wagonjwa na waliojeruhiwa wanatibiwa, mradi sio malengo ya kijeshi, kuelekeza mashambulizi kwa makusudi dhidi ya raia kama hivyo, au dhidi ya raia binafsi waoshiriki moja kwa moja katika uhasama, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashambulizi ya kiholela na kusababisha kifo au majeraha kwa raia na kuanzisha mashambulizi yasiyo na uwiano kwa makusudi, pia ni uhalifu wa kivita, ripoti hiyo inaongeza.
Katika hali fulani, uharibifu wa makusudi wa vituo vya huduma ya afya unaweza kuwa aina ya adhabu ya pamoja, ambayo pia inaweza kujumuisha uhalifu wa kivita.
Ripoti hiyo pia inabainisha kuwa baadhi ya vitendo hivi, kama vimefanywa kama sehemu ya shambulio lililoenea au la kimfumo dhidi ya raia, zaidi kwa serikali au, ikiwa ni mhusika asiye wa serikali, sera ya shirika, inaweza pia kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Ripoti inasema katika baadhi ya mashambulio hayo, huenda wanajeshi wa Israel walitumia silaha nzito na mabomu ya angani yenye madhara makubwa. Inaonekana kwamba risasi ya MK 83 ilitumiwa katika shambulio la anga la Januari 10 2024 mbele ya Hospitali ya Mashahidi wa Al Aqsa huko Deir Al-Balah, Gaza ya Kati. Pia inasemekana kwamba watu wasiopungua 12 waliuawa, akiwemo mwandishi wa habari na watu kadhaa waliokimbia makazi yao (IDPs), na watu 35 walijeruhiwa.
Utumiaji wa silaha za milipuko zenye athari za eneo pana katika eneo lenye watu wengi huibua wasiwasi mkubwa wa mashambulio ya kiholela.
Ripoti hiyo imegundua kuwa kipengele kingine cha mashambulizi kama hayo kimekuwa ni kulengwa kwa watu ndani ya hospitali, lakini kwamba katika visa vingi hivi ilikuwa vigumu kuamua kuhusika.
Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kesi nyingi za watu waliouawa kwa kupigwa risasi katika Hospitali ya Al Awda huko Jabalya, ikiwa ni pamoja na muuguzi wa kujitolea ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akichungulia dirishani 7 Desemba 2023.
@@@
Tukiwa bado katika kadhia hiyo ya sekta ya tiba ya Gaza, Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametangaza kwamba mfumo wa afya na matibabu wa Gaza umeporomoka, akisema: juhudi zote za shirika hili kwa ajili ya kuhifadhi mfumo wa afya katika Gaza zimeenda na maji.
Daktari Margaret Harris amesisitiza kwamba: Mashambulizi ya Israeli dhidi ya hospitali, wafanyakazi wa afya na wagonjwa hayawezi kukubalika katikka hali yoyote na yanapaswa kusitishwa.
Utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kupuuza sheria na maonyo yote ya kimataifa ya mashirika ya kimataifa, umelenga na kuharibu miundombinu ya afya na matibabu na aghalabu ya vituo vya afya na hospitali za Ukanda wa Gaza. Shambulio dhidi ya Hospitali ya Kamal Adwan na kuteketezwa kwake siku chache zilizopita, ni mfano wa hivi karibuni katika suala hili.
Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa Shirika la Afya Duniani, akiashiria utawala wa Kizayuni wa Israel, ameandika katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Hospitali za Gaza zimekuwa uwanja wa vita, na mfumo wa afya unakabiliwa na tishio kubwa. Sitisha mashambulizi dhidi ya hospitali. Watu wa Gaza wanahitaji kupata huduma za matibabu. Waokoaji wanahitajikka ili kutoa usaidizi wa kiafya. Sitisha mapigano."
Tangu kuanza kwa vita vya Gaza, utawala wa Kizayuni umeshaua shahidi zaidi ya madaktari na wauguzi elfu moja wa Kipalestina katika mashambulizi ya makusudi dhidi ya wafanyakazi wa afya katika Ukanda wa Gaza, na zaidi ya wafanyakazi 300 wa matibabu wamekamatwa na kuteswa. Takwimu zinaonyesha kuwa hospitali 34 zimeshambuliwa kutokana na mashambulizi ya Israel na vituo 80 vya afya vimeharibiwa kabisa.
Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina linasema hadi hivi karibuni ni hospitali tatu tu ndizo zilikuwa zikifanya kazi kaskazini mwa Gaza ya mwisho ikiwa ni Hospitali ya Kamal Adwan.
Kwa mazingira haya, hali sasa imekuwa ngumu zaidi kwa wakazi wa Gaza. Pamoja na kuporomoka kwa mfumo wa matibabu, hali ya hewa ya baridi, na ukosefu wa vituo vya afya, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu kumeongezeka, na wagonjwa wengi wanaohitaji matibabu endelevu wanashindwa kuendelea na matibabu yao.
Munir Al-Barsh, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Gaza, alieleza katika taarifa yake kile kinachotokea kaskazini mwa Gaza kuwa mauaji ya kimbari, ambayo yanaonyesha kushindwa kwa dhamiri ya binadamu. Alisema: "Kinachotokea Gaza leo kinapita zaidi ya jinai za kawaida na ni mauaji ya kimbari kwa maana yake kamili, yanayotekelezwa mbele ya macho ya walimwengu."
@@@
Naam tuliyoyataja leo ni sehemu ndogo tu kuhusu ulivyoporomoka mfumo wa afya katika Ukanda wa Ghaza eneo ambalo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza mauaji ya kimbari.