Dec 15, 2016 04:13 UTC
  • Alkhamisi, 15 Disemba, 2016

Leo ni Alkhamisi tarehe 15 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1438 Hijria sawa na tarehe 15 Disemba mwaka 2016.

Siku kama ya leo miaka 41 iliyopita, yaani tarehe 15 Disemba 1975, zilimalizika zama za udhibiti na ushawishi wa Uhispania huko Sahara ya Magharibi baada ya nchi hiyo kulazimika kuondoka katika eneo hilo. Polisario ni moja ya harakati za ukombozi wa Sahara Magharibi zilizowalazimisha Wahispania kukimbia eneo hilo. Harakati hiyo iliundwa mwaka 1973 baada ya wanamapinduzi wa Sahara kuasisi makundi kadhaa ya kupigania ukombozi wa eneo hilo.

Bendera ya Jamhuri ya Sahara Magharibi 

Miaka 500 iliyopita katika siku kama hii ya leo, makundi ya kwanza ya wahamiaji wa Kihispania yaliwasili Argentina mwaka mmoja baada ya kugunduliwa pwani ya nchi hiyo ya Amerika ya kusini. Kuwasili kwa wahamiaji hao ulikuwa mwanzo wa utawala wa Uhispania nchini Argentina. Ukoloni wa Uhispania huko Argentina ulifikia kikomo mwaka 1917 kufuatia mapambano ya ukombozi ya wananchi wa nchi hiyo.

Na siku kama ya leo miaka 164 iliyopita alizaliwa mwanafikizia wa Kifaransa Henri Becquerel. Henri ambaye ndiye aliyevumbua nururishi au Radioactivity baada ya kufanya utafiti katika mada za urani na vitu vinginevyo, alianza kufanya jitihada za kupata vitu vinavyotoa miali ya X baada ya miali hiyo kugunduliwa na mwanafizikia wa Kijerumani, Wilhelm Conrad Röntgen 8 November 1895. Mwaka 1896 Becquerel aligundua nururishi  inayoweza kuzalisha miali ya X. Utafiti wa mwanafikizia huyo wa Kifaransa ulimfanya atunukiwe tuzo ya Nobel mwaka 1903. Msomi huyo alifariki dunia mwaka 1908. 

Henri Becquerel