Apr 21, 2018 11:07 UTC
  • Jumamosi, 21 Aprili, 2018

Leo ni Jumamosi tarehe 4 Shaaban 1439 Hijria sawa na tarehe 21 Aprili 2018 Miladia.

Leo tarehe Mosi Ordibehesht katika kalenda ya mwaka wa Hijria Shamsia ni siku ya kumuenzi Sheikh Muslihuddeen Saadi Shirazi malenga, mshairi na mwalimu stadi wa tungo za mashairi na nathari wa Kifarsi. Saadi Shirazi alizaliwa karibu mwaka 606 Hijria Qamariya katika familia ya kielimu kwenye mji wa Shiraz ulioko kusini mwa Iran na baada ya kukipitisha kipindi cha utoto na kuinukia kwake katika mji alikozaliwa wa Shiraz nchini Iran, akiwa kijana Saadi Shirazi aliamua kwenda katika mji wa Baghdad huko Iraq. Akiwa huko alisoma katika shule ya Nidhamiya na baadaye kufanya safari katika maeneo ya Sham, Hijaz, Roma na katika maeneo mengine. Katika safari zake hizo, malenga huyo mashuhuri alifanikiwa kufahamiana na jamii mbalimbali na kuona mengi yaliyoimarisha kipawa chake cha kutunga mashairi. Saadi Shirazi ni miongoni mwa malenga na washairi wakubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Saadi Shirazi ameandika vitabu kadhaa, muhimu zaidi ni kile cha tungo cha Bustan na kitabu chake cha nathari cha Golestan. ***

Sheikh Muslihuddeen Saadi Shirazi

Katika siku kama ya leo miaka 1413 iliyopita, yaani tarehe 4 Shaaban mwaka 26 Hijria, alizaliwa Abbas bin Ali bin Abi Talib mashuhuri kwa lakabu ya Abul Fadhl. Mama yake ni Ummul Baniina, ambaye aliolewa na Imam Ali bin Abi Twalib (A.S) baada ya kufariki dunia bibi Fatima Zahra AS. Alikulia katika familia ya watu adhimu kama baba yake Ali (as) kaka zake Imam Hassan na Hussein na dada yake mukufu Zaunab (as). Alimpenda sana kaka yake Hussein Bwana wa mashahidi kiasi kwamba alisabilia roho na nafsi yake katika ardhi ya karbala akimtetea yeye na risala yake. Abbas alifahamika mno kutokana na elimu, ukweli na uchaji Mungu wake. Kutabahari kwake kielimu kuliwafanya watu wengi warejee kwa ajili ya kutatuliwa masuala mbalimbali ya kielimu. Siku ya kuzalwia Abul Fadhl Abbas inatambuliwa hapa nchini kama Siku ya Vilema wa Vita. ***

Kuzaliwa Abul-Fadhl

Miaka 1189 iliyopita katika siku kama ya leo, Egbert Mfalme wa Kwanza wa Uingereza alichukua madaraka baada ya vita vya muda mrefu. Kabla ya hapo Uingereza ilikuwa ikiongozwa na wafalme wa kiukoo huku ikiwa imegawika katika sehemu kadhaa za kijiografia na kila mtawala akitawala eneo lake maalumu. Egbert aliyekuwa mfalme wa Wessex, eneo lililokuwa Kusini mwa Uingereza ya sasa, baada ya kupambana na watawala wa kitabaka na kuwashinda, mwaka 829 alifanikiwa kushika madaraka akiwa Mfalme wa Kwanza wa Uingereza na kuasisi silsila ya utawala wa Wasaxoni wa Magharibi. ***

Egbert

Na siku kama ya leo miaka 80 iliyopita, Allamah Muhammad Iqbal Lahori mwanafikra, mwanafalsafa na malenga wa Kiislamu aliaga dunia huko Bara Hindi. Alizaliwa mwaka 1873 katika mji wa Sialkot kwenye jimbo la Punjab. Baada ya kumaliza masomo ya awali na ya juu na kupata shahada ya uzamili, Allamah Muhammad Iqbal Lahori alielekea nchini Ujerumani na baadaye Uingereza kwa lengo la kujiendeleza katika elimu ya falsafa na kubaki huko kwa kipindi cha miaka minne. Malenga huyo alianza kutunga mashairi akiwa katika masomo yake ya sekondari. Baada ya kurejea India, Iqbal Lahori alianza kuwaamsha Waislamu wa nchi hiyo na kufanya jitihada za kuwaunganisha pamoja huku akibainisha fikra na mitazamo yake kupitia beti za mashairi. Mwanafalsafa huyo anahesabiwa kuwa mmoja wa waanzilishi na waasisi wa Pakistan huru. ***

Mohamed Iqbal Lah