Dec 15, 2021 02:28 UTC
  • Jumatano tarehe 15 Disemba 2021

Leo ni Jumatano tarehe 10 Jamadil Awwal 1443 Hijria sawa na Disemba 15 mwaka 2021.

Miaka 506 iliyopita katika siku kama hii ya leo, makundi ya kwanza ya wahamiaji wa Kihispania yaliwasili Argentina mwaka mmoja baada ya kugunduliwa pwani ya nchi hiyo ya Amerika ya kusini. Kuwasili kwa wahamiaji hao ulikuwa mwanzo wa utawala wa Uhispania nchini Argentina. Ukoloni wa Uhispania huko Argentina ulifikia kikomo mwaka 1917 kufuatia mapambano ya ukombozi ya wananchi wa nchi hiyo.

Siku kama ya leo miaka 169 iliyopita alizaliwa mwanafikizia wa Kifaransa Henri Becquerel. Henri ambaye ndiye aliyevumbua nururishi au Radioactivity baada ya kufanya utafiti katika mada za urani na vitu vinginevyo, alianza kufanya jitihada za kupata vitu vinavyotoa miali ya X baada ya miali hiyo kugunduliwa na mwanafizikia wa Kijerumani, Wilhelm Conrad Röntgen 8 November 1895. Mwaka 1896 Becquerel aligundua nururishi  inayoweza kuzalisha miali ya X. Utafiti wa mwanafikizia huyo wa Kifaransa ulimfanya atunukiwe tuzo ya Nobel mwaka 1903. Msomi huyo alifariki dunia mwaka 1908. 

Henri Becquerel

Miaka 65 iliyopita muwafaka na leo alifariki dunia Walt Disney shakhsiya mashuhuri wa sekta ya filamu za watoto. Disney alizaliwa mwaka 1901 huko Marekani. Walt Disney alihitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Havard na kutunukiwa shahada ya udaktari katika sayansi ya uchoraji na uchongaji (Fine Art). Disney alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha sanaa ya filamu za katuni. Mara kadhaa alitunukiwa tuzo za Oscar katika uwanja huo wa kutengeneza filamu za katuni.

Walt Disney

Na miaka 46 iliyopita katika siku kama hii ya leo yaani tarehe 15 Disemba 1975, majeshi ya kikoloni ya Uhispania yalianza kuondoka Sahara Magharibi.  Polisario ni moja ya harakati za ukombozi wa Sahara Magharibi iliyowalazimisha Wahispania kukimbia eneo hilo. Harakati hiyo iliundwa mwaka 1973 baada ya wanamapinduzi wa Sahara kuasisi makundi kadhaa ya kupigania ukombozi wa eneo hilo.

Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sahara Magharibi

 

Tags