Nov 20, 2022 07:17 UTC
  • Hakika ya Uwahabi 4

Katika kitabu chake chenye kurasa 1,400 na alichokipa anwani ya "Historia ya Aal Saud", Nasser as-Saeed anafichua siri ambayo pengine hakuna mtu mwingine yeyote aliyeizingatia hapo awali.

Bismillahir Rajmanir Raheem.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Aya ya 82 ya Surat al-Maida:

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walioamini ni Mayahudi na washirikina.

Assalaam Alaykum Wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayokutanagazieni kutoka mjini Tehran. Mtakumbuka kuwa katika vipindi vitatu vilivyopita tuliazungumzia historia fupi ya kubuniwa utawala wa Mawahabi huko Saudi Arabia. Tuliona jinsi Uingereza na majasusi wake walivyoanzisha urafiki na muungano wa kiutawala kati ya ukoo wa Saud na familia ya Muhammad bin Abdul Wahhab. Tulisema kuwa baada ya kumalizika Vita vya Kwanza vya Dunia ambapo utawala wa Othmania na washirika wake walishindwa na kusambaratishwa, Uingereza ilizipa koo mbili hizo fedha na silaha nyingi kwa ajili ya kuendesha mauaji makubwa na ya kutisha dhidi ya watawala na watu wa Bara Arabu. Baada ya kuimarisha utawala wao katika eneo hilo, walibadilisha jina lake na kulipa jina la ukoo wao yaani Saudi Arabia. Baada ya kudhibiti ardhi hiyo Mawahabi na washirika wao wa ukoo wa Aal Saud walifanya mauaji ya kutisha na kuharibu kabisa turathi na ustaarabu wa kale na mpya wa ulimwengu wa Kiislamu. Swali muhimu la kujiuliza hapa ni kwamba, je, ni kwa nini Uingereza ulizachagua koo mbili hizo kwa ajili ya kufikia malengo yake katika jamii na nchi za Kiislamu? Iliona kitu gani cha kuvutia katika koo hizo na hivyo kuwatuma majasusi wake ili kwenda kuzishawishi zishirikiane nao katika malengo yao maovu dhidi ya Umma wa Kiislamu?

***********

Huenda tukapata majibu ya maswali hayo katika kitabu kilichoandikwa na Nasser as-Saeed, mwandishi mashuhuri wa Saudi Arabia. Anafichua katika kitabu chake hicho chenye kurasa 1,400 alichokipa anwani ya "Historia ya Aal Saud" siri ambayo pengine hakuna mtu mwingine yeyote aliizingatia hapo awali. Katika kurasa 30 za mwanzo za kitabu hicho, anachambua na kufafanua kwa kina shajara ya ukoo wa kifalme wa Mawahabi na Wasaudia. Kwa kutumia uthibitisho wa nyaraka na dalili za kihistoria, Nasser as-Saeed anasema kwamba asili ya koo hizo inatokana na Mayahudi waliokuwa wakiishi katika ardhi ya Hijaz na hasa katika mji wa Madina. Baada ya kuchapisha kitabu hicho, Nasser as-Saeed aliuawa kigaidi na vibaraka wa Aal Saud na kwa amri yao ya moja kwa moja.

Shahidi Nasser as-Saeed

Mtu mwingine aliyefanya utafiti wa kina na kukiri kwamba mababu wa Mawahabi walikuwa Mayahudi ni Ali al-Shueibi. Huyu ni mwanafikra mwenye asili ya Syria ambaye alifanya kazi katika uwanja wa Mawahabi kwa muda mrefu wa miaka ishirini na alikuwa mshauri wa Mfalme Fahd kati ya mwaka 1983 hadi 1989. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Ali al-Shueibi alipata kujua zaidi fikra za Imam Khomeini (Ma) mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu na za Kishia na taratibu akaanza kukosoa fikra na mitazamo ya Ibn Taymiyyah na Muhammad bin Abd al-Wahhab. Alichapisha kitabu kiitwacho "Islamic Thoughts with a Modern View" na kutenga juzuu mbili za kitabu hicho chenye juzuu mia moja katika kukosoa fikra za Uwahabi. Ali al-Shuaibi, ambaye aliachana na itikadi ya Uwahabi na kukubali madhehebu ya Shia mwaka 1987, anaamini kwamba babu wa nne wa Muhammad bin Abd al-Wahhab pia alikuwa Myahudi kutoka mji wa Izmir nchini Uturuki.

Ali as-Shueibi

***********

Qassem Hossein al-Zein ni mwandishi mwingine wa Kiarabu ambaye ameandika kitabu kinachoitwa "Nyoka wa Changarawe Inayotiririka". Anaanza kuandika kitabu chake kwa kukumbuka safari iliyofanywa na John Philippi huko Najran. John Philippi, mshauri wa Kiingereza wa Mawahabi, aliingia Najran akiwa ameandamana na mmoja wa marafiki zake anayeitwa Muhammad al-Tamimi, ambaye baadaye alipewa jukumu la kuandika nasaba (shajara) ya familia ya Aal Saud. Walitumwa huko kufikisha zawadi ya Mfalme wa Kiwahhabi Abd al-Aziz kwa familia ya Kiyahudi ya Yusuf bin Muqrin na kukidhi mahitaji yake ya kifedha. Yusuf bin Muqrin pia alimtumia Mfalme Abd al-Aziz hati ya lugha ya Kiebrania na Kiarabu akimshukuru kuhusu zawadi aliyomtumia. Maandishi hayo yaliyoandikwa chini ya anwani ya "Chemichemi Inayobubujika ya Najran katika Urithi wa Wakazi Wake wa Kwanza", yalikuwa na habari muhimu kuhusu mababu wa ukoo wa Masaudi na Mawahabi.

John Philippi akiwa amevalia vazi la Kiarabu

Baadaye, John Philippi aliandika kitabu kinachoitwa "Nyakati za Waarabu" ambapo alibainisha kwamba kwa mujibu wa maandishi ya "Yusuf bin Muqrin" jina halisi la ukoo wa Aal Saud ni "al Mordechai". Vyanzo kadhaa vimemtambua babu wa ukoo wa Masaudi na Mawahabi  kuwa Myahudi wa Kituruki anayeitwa Mordechai Ibn Ibrahim Ibn Moshe. Wanahistoria wengi wanakubali kwamba ukoo wa Masaudi unarudi nyuma hadi kwa Mayahudi wa Basra. Mayahudi wa Basra kimsingi ni wale waliokimbia Hispania mwishoni mwa karne ya 15 kufuatia hatua za Mahakama za Kudadisi Itikadi nchini humo na kwenda kuishi Istanbul nchini Uturuki, ambapo baadaye waliamua kuhamia mjini Basra katika Iraq ya leo. Waliepuka mateso na ukandamizaji kwa kuficha imani yao ya Uyahudi na kuchanganyika na jamii za wenyeji wa mji huo. Muonekano wao ulikuwa ni kwamba walivaa kofia nyekundu, kuweka ndevu ndefu na kunyoa vichwa vyao. Ni muonekano huo tofauti ndio uliowapelekea wajulikane kama "Wajukuu wa Kofia Nyekundu" au "al-Tarabish al-Hamra" miongoni mwa Waarabu. Kulingana na vyanzo vingine, "al-Tarabish al-Hamra" ni jina lile lile ambalo wanawafalme wa Kiwahabi wa Saudia huitana wanapokuwa kwenye mazungumzo yao maalumu.

*************

Ukweli kwamba mwanzoni mwa kudhihiri Uislamu huko Uarabuni, kulikuwa na makabila mengi ya Mayahudi walioishi karibu na Madina ni jambo linalojulikana na kila mtu, Mayahudi ambao, kulingana na kitabu chao cha mbinguni, walikuwa wakisubiri kudhihiri kwa nabii mpya na wakitambua vizuri pia ishara zake. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 146 ya Sura al-Baqarah: "Wale tuliowapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao; na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua."

Mtume wa Uislamu alipobaathiwa, badala ya Mayahudi wa Madina kumkubali pamoja na ujumbe aliotumwa nao walimpinga na wakawa miongoni mwa maadui zake wakubwa. Walipanga na kuanzisha vita vingi dhidi ya Uislamu, na hata walikuwa na nafasi kubwa katika kuendesha vita vingi vya washirikina dhidi ya Mtume (saw). Bani Nadhir, Bani Quraydha" na Bani Qainuqah walikuwa miongoni mwa Mayahudi waliokuwa wakiishi katika viunga vya mji wa Madinah, na kabila la kwanza la Mayahudi lililovunja mkataba wa amani na Mtume (saw) lilikuwa ni kabila la "Bani Qainuqah." Baada ya Vita vya Badr, Mtume  (saw) aliwakabili Mayahudi waliovunja mapatano ya Madina, akawapiga vita na kuwashinda. Ingawa alishinda katika uwanja wa vita lakini hakuwatoa roho wala kuwakandamiza maadui zake bali aliwafukuza kutoka Madina. Baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba miongoni mwa Mayahudi hao waliofukuzwa kutoka Madina na Mtume Mtukufu (saw) ni mababu wa Mawahabi wa Saudi Arabia.

*************

 

Mbali na yale yote yanayosemwa na baadhi ya watu kuhusu mababu wa Kiyahudi wa Mawahabi, lakini wafalme wa Saudia wenyewe baadhi ya wakati hukiri kuhusu asili yao ya Kiyahudi. Mfalme Salman, wakati mmoja alipokuwa akizungumzia wafalme wa zamani wa Kisaudi na Kiwahabi, alisema: "Eeh Mwenyezi Mungu! Warehemu wafalme wa Kiyahudi waliotangulia kabla yangu." Kwa kauli hii, alikiri waziwazi na kujivunia Uyahudi wake.

Mfalme Faisal na Bin Salman, katika mahojiano ya wazi au katika mazungumzo ya faragha, wamekiri kwamba wao na familia zao ni Mayahudi, jambo ambalo liliwavutia sana Wazayuni kiasi kwamba hawakuweza kuficha furaha yao kuhusu jambo hilo. Mike Evans, mwanzilishi na mkuu wa Kituo cha Urithi wa Marafiki wa Kiyahudi, ambao ni wakala wa Kizayuni unaounga mkono utawala wa Tel Aviv, alisema katika mkutano wa kila mwaka wa gazeti la The Jerusalem Post mnamo 2019: "Nilipokutana na Mwana Mfalme wa Saudia, nilimuuliza mtazamo wake kuhusu Mayahudi na Wakristo. Naye akajibu: Nawapenda wote wawili. Nilipomuuliza sababu ya kufanya hivyo alisema: Kwa sababu mama yangu alitokana na moja ya makundi hayo! Mkuu wa nyumba ya baba yangu, ambaye alinilea, alikuwa Myahudi Muevanjilisti kutoka Ethiopia."

 

Licha ya kukiri kote huko lakini sera jumla za ukoo wa Aal Saud zimejengeka katika msingi wa kukana ukweli huo na kuficha uhusiano wake na Mayahudi. Sambamba na sera hizo, Mfalme Abdul Aziz alimuagiza Muhammad Al-Tamimi kuandika nasaba ya uwongo ambayo ingebuni na kuonyesha kuwepo mfungamano wa ukoo wa Aal Saud na Mtume Muhammad (saw). Muhammad Al-Tamimi ndiye yule yule aliyeenda kumtembelea binamu wa Kiyahudi wa Mawahhabi akiwa pamoja na John Philippi. Malipo ya huduma hiyo nzuri kwa Mawahabi ilikuwa ni Mohammad Al-Tamimi kukabidhiwa vyeo muhimu katika Ufalme wa Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na kupewa usimamizi wa maktaba za umma katika ufalme huo. Al Saud wanasahau kwamba mtu yeyote ambaye ni mtenda dhambi na kafiri hawezi kujinasibisha kwa Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad (saw), hata kama ana uhusiano wa damu wa karibu kiasi gani na Mtume wa Uislamu (saw). Katika Uislamu, Bilal Habashi, ingawa alikuwa mtumwa mweusi, lakini aliheshimika zaidi mbele ya Mtume (saw) kutokana na ucha-Mungu wake kuliko waabudu masanamu kama Abu Lahab, ambaye alikuwa ami yake Mtume (saw).