-
Iran yatungua ndege 2 za kivita za Israel za F-35, yamkamata rubani
Jun 14, 2025 07:05Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimefanikiwa kutungua na kuteketeza ndege mbili za kivita za Israel aina ya F-35, na idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani. Iran imekuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kutungua ndege ya kijeshi ya F-35.
-
Jenerali Hatami ateuliwa kuwa Kamanda mpya wa Majeshi ya Iran
Jun 14, 2025 07:04Brigedia Jenerali Amir Hatami ameteuliwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kuwa Kamanda Mkuu mpya wa Majeshi ya Iran.
-
Tehran: Mazungumzo ya nyuklia na US 'hayana maana' baada ya uvamizi wa Israel
Jun 14, 2025 06:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran "hayana maana" kufuatia mashambulizi ya kinyama ya Israel, huku akiishutumu Washington kwa kuunga mkono uchokozi huo.
-
Iran: EU ikishinikiza turejeshewa vikwazo vya UN, tutajitoa NPT
Jun 12, 2025 02:53Iran imeonya kwamba, huenda ikatumia haki yake ya kisheria ya kujiondoa kwenye Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) ikiwa mataifa ya Ulaya yataendelea na jaribio lisilo na msingi wa kisheria la kuamilisha mchakato wa kurejeshwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Je, mashirikiano ya Iran na Afrika yataimarika vipi?
Jun 12, 2025 02:09Katika kikao chao na Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, mabalozi wa Senegal na Sierra Leone wamesisitiza utayari wa nchi za Kiafrika kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Iran.
-
Iran: Tutapiga vituo vya siri vya nyuklia vya Israel iwapo tutashambuliwa
Jun 10, 2025 03:03Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) limeonya kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itavishambulia vituo vya siri vya nyuklia vya Israel iwapo utawala huo wa Kizayuni utafanya kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya taifa hili.
-
Iran: Ni kwa manufaa ya US kulichukulia kwa uzito pendekezo letu
Jun 09, 2025 11:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei amesema Tehran hivi karibuni itawasilisha pendekezo lake kuhusu makubaliano ya nyuklia kupitia Oman, akitoa wito kwa Washington kutopoteza fursa hii, na kulichukulia kwa uzito pendekezo la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran: Vikwazo vya US dhidi ya majaji wa ICC vinakirihisha
Jun 09, 2025 02:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei amekosoa vikali hatua ya Marekani ya kuwawekea vikwazo majaji wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutokana na uchunguzi wao juu ya uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Iran, Imarati zasisitiza haja ya Waislamu kote duniani kuwa na umoja
Jun 07, 2025 07:00Rais Masoud Pezeshkian wa Iran na Kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan wametoa wito wa umoja wa Waislamu.
-
Pezeshkian: Umoja wa mataifa ya Kiislamu ni wajibu wa kidini na kistratajia
Jun 05, 2025 06:54Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu inatazama umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa ya Kiislamu kuwa ni wajibu wa kidini na wa kimkakati.