-
Msalaba Mwekundu: Mamia ya Wakongomani wamekimbilia Uganda
Jan 02, 2019 11:46Shirika la Msalaba Mwekundu limesema mamia ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchini Uganda baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Jumapili iliyopita.
-
Zoezi la kuhesabu kura laendelea DRC
Jan 02, 2019 04:16Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku huduma ya intaneti na ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) zikiwa bado zimekatwa kote nchini humo.
-
Kongo yakata huduma ya intaneti kwa siku ya pili kuzuia machafuko kabla ya matokeo ya uchaguzi
Jan 01, 2019 11:45Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekata huduma ya intaneti na ujumbe wa mfupi wa simu za mkononi wa SMS kote nchini humo kwa siku ya pili mfululizo hii leo wakati nchi hiyo ikisubiri kwa hamu kubwa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais.
-
Wapinzani Kongo DR walalamikia ukiukwaji mkubwa wa taratibu katika uchaguzi wa rais
Dec 31, 2018 04:35Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamedai kuwa uchaguzi wa jana Jumapili ulikumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo za kukwama kwa mashine za kupigia kura, mvua kubwa katika maeneo mengi pamoja na machafuko na vurugu.
-
Uchaguzi DRC: Wakazi wa Beni wafanya uchaguzi wa mwigo
Dec 30, 2018 11:45Licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo CENI kuakhirisha uchaguzi katika maeneo matatu ya nchi hiyo ya Beni, Butembo na Yumbi kutokana na ugonjwa wa Ebola na mapigano ya kikabila, lakini maelfu ya wakazi wa mji wa Beni hii leo wamepanga foleni na kushiriki uchaguzi wa mwigo, wakiwa na lengo la kuidhihaki tume hiyo.
-
Uchaguzi Mkuu DRC katikati ya changamoto za kiusalama na mivutano ya kisiasa
Dec 30, 2018 10:10Uchaguzi Mkuu wa Rais na Bunge wa Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo umefanyika leo Jumapili Disemba 30, 2018 huku mvua kali ikinyesha. Uchaguzi huo umefanyika chini ya changamoto nyingi za kiusalama na kisiasa.
-
Uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu waanza Kongo
Dec 30, 2018 04:36Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong leo Jumapili wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura katika uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu nchini humo. Uchaguzi huo wa leo huwenda ukawa wa kwanza wa kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko.
-
Uchaguzi mkuu wa Kongo na changamoto zinazoikabili nchi hiyo
Dec 29, 2018 07:39Uchaguzi mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hatimaye utafanyika kesho Jumapili baada ya kuakhirishwa mara kadhaa. Raia wa nchi hiyo kesho Jumapili tarehe 30 Disemba wataelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kumchagua mrithi wa Rais Joseph Kabila licha ya kuendelea mivutano ya kisiasa nchini humo.
-
Katibu Mkuu wa UN ataka uchaguzi huru na wa haki Kongo DR
Dec 29, 2018 04:45Huku wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotimiza masharti ya kupiga kura wakitazamiwa kuelekea katika masanduku ya kupigia kura kumchangua kiongozi atakayerithi mikoba ya Rais Joseph Kabila Jumapili ya kesho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa pande zote husika za kisiasa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa uhuru na amani.
-
Martin Fayulu, mgombea wa upinzani aongoza katika kura ya maoni DRC
Dec 28, 2018 12:34Utafiti mpya wa maoni umeonesha kuwa mgombea wa muungano wa upinzani wa Lamuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Martin Fayulu ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika Jumapili ijayo.