Uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu waanza Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50517-uchaguzi_wa_rais_ulioakhirishwa_kwa_muda_mrefu_waanza_kongo
Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong leo Jumapili wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura katika uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu nchini humo. Uchaguzi huo wa leo huwenda ukawa wa kwanza wa kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko.
(last modified 2025-12-01T10:34:25+00:00 )
Dec 30, 2018 08:06 UTC
  • Uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu waanza Kongo

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong leo Jumapili wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura katika uchaguzi wa rais ulioakhirishwa kwa muda mrefu nchini humo. Uchaguzi huo wa leo huwenda ukawa wa kwanza wa kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko.

Habari zinasema kuwa kuna wasiwasi wa kutokea ghasia katika zoezi la leo la uchaguzi wa rais baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwazuia watu karibu milioni moja kupiga kura kwa sababu ya mlipuko wa homa ya Ebola iuioiathiri mikoa ya mashariki mwa nchi hiyo. Uamuzi huo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kongo umekosolewa pakubwa kwa sababu unaweza kuibua alama ya kuuliza kuhusu uhalali wa uchaguzi wa leo nchini nchini humo.

Wagombea wakuu wa kiti cha urais kutoka  upande wa upinzani ni Martin Fayulu na Felix Tshisekedi ambao wanachuana na Emmanuel Ramazani Shadary mgombea wa chama tawala anayeuungwa mkono na Rais Joseph Kabila. Shadary alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kongo. Ramazani Shadary pia anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya.  

Emmanuel Ramazani Shadary, mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama tawala 

Hii ni mara ya kwanza ambapo wapiga kura milioni 40 nchini Kongo wanatumia mashinde za kielektroniki kupiga kura na wapinzani wanasema kuwa wana wasiwasi na mfumo huo wa upigaji kura kwa sababu matokeo yanaweza kuchakachuliwa. Wakati huo huo baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi nchini Kongo wamesema kuwa vifaa vya kupigia kura vimechelewa kufika katika vituo vya kupigia kura.