-
Wanaharakati Kenya wataka haki itendeke baada ya mume kumkata mikono mkewe kwa panga
Aug 02, 2016 11:53Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake nchini Kenya wametaka nguvu zote za sheria zitumike dhidi ya mume aliyemkata mikono mke wake kwa panga kwa sababu hajamzalia mtoto ili liwe funzo kwa wahusika wengine wa vitendo vya ukatili wa majumbani nchini humo.
-
Shule zaendelea kuchomwa Kenya, wasiwasi watanda
Jul 29, 2016 12:33Vitendo vya kuchoma moto shule vinavyoshadidi kila uchao huko Kenya vimeitia wasiwasi mkubwa serikali ya nchi hiyo.
-
UNHCR: Maelfu ya wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya wamerejea kwao kwa hiari
Jul 29, 2016 03:35Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, maelfu ya wakimbizi wa Somalia huko nchini Kenya wamerejea kwao kwa hiari.
-
UN: Wakenya 42,000 walikuwa wakimbizi 'bandia' Dadaab
Jul 27, 2016 03:24Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa, Wakenya 42,000 wamekuwa wakijifanya wakimbizi katika kambi ya Dadaab kwa shabaha ya kufaidika na misaada ya kibinadamu.
-
Ripoti: Uganda yaongoza kwa visa vya uhalifu Afrika Mashariki
Jul 26, 2016 12:25Utafiti mpya umefichua kuwa, Uganda ndiyo inayoongoza kwa visa vya uhalifu wa kutumia silaha za moto katika kanda ya Afrika Mashariki.
-
Pasta aliyebaka na kuua nchini Kenya akutwa na hatia
Jul 21, 2016 23:33Pasta wa kanisa moja la kipendekosti nchini Kenya anasubiria hukumu ya kifo dhidi yake baada ya mahakama ya nchi hiyo hapo jana Alkhamis kumkuta na hatia ya kumuua muumini wake baada ya kumbaka.
-
Shrika la Muhuri: Kenya inakabiliwa na tatizo kubwa la mauaji ya kiholela
Jul 20, 2016 23:56Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Muslims for Human Rights (Muhuri) nchini Kenya, Hassan Abdi Abdille amesema kuwa, wimbi la kutoweka kwa watu na kisha kupatikana baadaye wakiwa wameuawa kikatili, limekuwa sugu na kwamba serikali haijachukua hatua za kisheria kuhusu suala hilo.
-
Iran, Kenya kuimarisha ushirkiano wa kiuchumi
Jul 19, 2016 23:33Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran Ali Tayebnia ameelezea matumaini kuwa, baada ya kuondolewa vizingti vya uhusiano wa kibenki, Kenya na Iran zitaweza kuimarisha uhusiano katika sekta za biashara na viwanda.
-
Usalama waimarishwa zaidi Nairobi Kenya huku mkutano wa UNCTAD ukiendelea
Jul 18, 2016 09:33Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi huku mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ukiendelea kufanyika mjini humo.
-
Mkutano wa UNCTAD wafunguliwa Nairobi, Kenya
Jul 18, 2016 00:33Mkutano wa 14 Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) uliofunguliwa jana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Nairobi umeanza kwa kutolewa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya nchi za dunia.