-
Mbunge wa UK: FIFA na UEFA zina 'nyuso mbili za ubaguzi wa rangi' kwa maslahi ya Israel
Nov 14, 2024 02:38Mbunge wa chama cha Leba nchini Uingereza Zarah Sultana amekosoa vikali mashirikisho ya juu ya soka duniani ya FIFA na UEFA kwa kutoziadhibu timu za soka za Israel wakati utawala huo wa Kizayuni unaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
UN: Nchi zinazohusika ziache kuzipatia silaha pande zinazopigana nchini Sudan
Nov 13, 2024 08:26Umoja wa Mataifa umesema, kuendelea kuwasambazia silaha askari wa jeshi na wa vikosi vya wanamgambo wanaopigana nchini Sudan ndiko "kunakowezesha kufanyika uchinjaji" na lazima kukomeshwe wakati raia wa nchi hiyo wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa vita.
-
Jumapili, 03 Novemba, 2024
Nov 02, 2024 22:58Leo ni Jumapili tarehe Mosi Mfunguo Nane Jamadul-Awwal 1446 Hijria mwafaka na 3 Novemba 2024 Miladia.
-
Iran yaendelea na jitihada za kusimamishwa vita Ghaza na Lebanon
Oct 31, 2024 03:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Misri, Indonesia na Qatar na kujadiliana nao masuala ya kikanda na uhusiano wa pande mbili ikiwa ni muondelezo wa jitihada za Iran za kuhakikisha vita vinakomeshwa huko Ghaza na Lebanon.
-
Iran na Misri zataka Israel ilazimishwe kukomesha jinai zake Gaza, Lebanon
Oct 24, 2024 02:48Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian na mwenzake wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi wamesisitiza kuwa uchokozi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon ni lazima usitishwe, na kutoa wito wa kuwepo juhudi za kuzuia kuenea kwa mzozo katika maeneo mengine ya eneo la Asia Magharibi.
-
Iran na Misri zajadili masuala ya kikanda na kimataifa
Oct 17, 2024 23:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi; ambapo wamejadili masuala muhimu ya kikanda na uhusiano wa pande mbili.
-
Marekani kuiuzia Misri makombora ya dola milioni 740
Sep 26, 2024 00:29Serikali ya Marekani imeidhinisha mauzo ya makombora yenye thamani ya mamilioni ya dola kwa Misri licha ya serikali ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kuendelea kuandamwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu.
-
Iran: Tuna haki ya kujibu mapigo ya mauaji ya kigaidi ya Haniyah
Aug 17, 2024 23:29Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ina haki ya kujibu kwa njia halali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumuua kigaidi Ismail Haniyah, aliyekuwa Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas akiwa ziarani hapa mjini Tehran.
-
Bagheri Kani: Iran itatoa jibu madhubuti kwa ugaidi wa Israel
Aug 07, 2024 03:36Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema utawala wa Israel ndio chanzo halisi cha ukosefu wa utulivu katika eneo la Asia Magharibi, na kwamba utawala huo wa Kizayuni unapata ujasiri wa kutenda jinai na vitendo vyake vya kigaidi kutokana na kimya cha nchi za Ulaya.
-
Makundi ya kisiasa Sudan yakataa kutia saini taarifa ya mwisho ya mkutano wa Cairo
Jul 08, 2024 03:37Mkutano wa makundi ya kisiasa na kiraia ya Sudan ulimalizika jana mjini Cairo, Misri ambapo vyama vya Sudan vilijadili njia za kutatua mgogoro wa ndani wa nchi hiyo, huku baadhi ya makundi yakikataa kutia saini taarifa ya mwisho ya mkutano wa Cairo.