Aug 07, 2024 07:06 UTC
  • Bagheri Kani: Iran itatoa jibu madhubuti kwa ugaidi wa Israel

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema utawala wa Israel ndio chanzo halisi cha ukosefu wa utulivu katika eneo la Asia Magharibi, na kwamba utawala huo wa Kizayuni unapata ujasiri wa kutenda jinai na vitendo vyake vya kigaidi kutokana na kimya cha nchi za Ulaya.

Ali Bagheri Kani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakata mzizi wa ukosefu wa usalama na ukosefu wa uthabiti katika eneo kwa "majibu yake madhubuti."

Bagheri Kani aliyasema hayo jana katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty na Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria, Alexander Schallenberg.

Bagheri Kani amejadiliana na mawaziri hao kuhusu mauaji ya Ismail Haniyah, Kiongozi wa Kisiasa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS, yaliyofanyika katika mji mkuu wa Iran Tehran, tarehe 31 Julai.

Iran imeulaumu utawala wa Israel kwa mauaji hayo, huku Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei akionya kuhusu "majibu makali" na kusisitiza tena wajibu wa Jamhuri ya Kiislamu wa kulipiza kisasi damu ya kiongozi huyo wa mapamabano.

Katika wito wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Bagheri amezungumzia matokeo mabaya ya kitendo cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni na matarajio kwenye kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

kabla ya hapo, mkuu wa chombo cha diplomasia wa Iran alisema katika mazungumzo ya simu na Peter Ciarto, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary ambaye nchi yake pia ni mwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Ulaya kuwa,  Tehran inapaswa kusimama kidete kukabiliana na utawala muovu kwa jina la utawala wa Kizayuni, ambao ndio chanzo cha ukosefu wa amani katika eneo.

Tags