-
Pua ya nguruwe na damu vyatapakazwa mbele ya msikiti Afrika Kusini
Jan 09, 2017 03:47Baraza la Sharia la Waislamu wa Afrika Kusini (MJC) limelaani kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kilichofanywa kwenye msikiti wa mji wa Simon katika jimbo la Cape Town cha kuweka pua ya nguruwe na kumwaga damu kwenye mlango wa msikiti huo.
-
Polisi ya Uganda yafanya msako katika msikiti wa Nakasero
Dec 27, 2016 23:21Kikosi cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Polisi nchini Uganda (JATT) jana Jumanne asubuhi kilifanya msako mkali katika msikiti wa Nakasero ulioko katika barabara ya Snay bin Amin jijini Kampala na kukamata watu kadhaa wakiwemo walinzi wa msikiti huo.
-
Kadhaa wajeruhiwa baada ya msikiti kuhujumiwa Zurich, Uswisi
Dec 20, 2016 04:33Watu watatu wamejeruhiwa baada ya mtu aliyekuwa na bunduki kushambulia msikiti na kufyatua risasi ovyo akiwalenga waumini waliokuwa wakitekeleza ibada zao katika mji wa Zurich nchini Uswisi usiku wa kuamkia leo.
-
Jumatatu, 12 Disemba, 2016
Dec 12, 2016 01:36Leo ni Jumatatu tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1438 Hijria sawa na Disemba 12, 2016.
-
Zaidi ya Misikiti 100 yahujumiwa nchini Uingereza, kuanzia Mei 2013
Nov 23, 2016 00:47Zaidi ya ya vituo vya Kiislamu na misikiti 100 imehujumiwa nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
-
Gaidi mmoja atishia kuripua msikiti mjini Michigan, Marekani
Oct 07, 2016 00:56Vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada vimezidi kuongezeka nchini Marekani, na habari za karibuni kabisa zinasema kuwa gaidi mmoja ametoa ametoa matamshi ya vitisho dhidi ya misikiti nchini humo.
-
Shambulio la kigaidi msikitini laua makumi ya watu Pakistan
Sep 16, 2016 22:10Watu wasiopungua 23 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililofanywa ndani ya msikiti katika Sala ya Ijumaa wilayani Mohmand nchini Pakistan.
-
Misikiti London yapokea vitisho kutoka magaidi wa mrengo wa kulia
Jul 09, 2016 23:10Misikiti kadhaa mjini London Uingereza imepokea vitisho vya kigaidi kutoka kwa makundi yanayoaminika kuwa ya wabaguzi wa mrengo wa kulia huku vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vikiongezeka nchini humo.
-
Watu wanane wauawa katika shambulizi msikitini Sudan
May 27, 2016 10:57Watu wanane wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa msikitini na watu waliokuwa na silaha katika mji wa al Junaynah mkoani Darfur Magharibi huko Sudan.
-
Waliovamia Msikiti Mwanza na kuua watu walikuwa na bendera za ISIS (Daesh)
May 20, 2016 11:57Genge la watu waliouhujumu msikiti mmoja wa mjini Mwanza kaskazini mwa Tanzania Jumatano usiku na kutekeleza mauaji walikuwa na bendera za kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.