Oct 07, 2016 04:26 UTC
  • Gaidi mmoja atishia kuripua msikiti mjini Michigan, Marekani

Vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada vimezidi kuongezeka nchini Marekani, na habari za karibuni kabisa zinasema kuwa gaidi mmoja ametoa ametoa matamshi ya vitisho dhidi ya misikiti nchini humo.

Gaidi huyo asiyejulikana ametoa vitisho hivyo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akipinga vikali mpango wa kujengwa msikiti na shule ya Kiislamu katika mji wa Pittsfield, jimbo la Michigan nchini Marekani.

Gaidi huyo mwenye chuki ya kupindukia dhidi ya dini ya Kiislamu ametishia kuuripua msikiti na shule hiyo endapo itajengwa mjini humo. Aidha ametoa maneno makali dhidi ya Waislamu na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani. 

Sehemu ya kikundi kinachoongoza chuki dhidi ya dini ya Kiislamu nchini Marekani.

Daud Walid, Mkurugenzi Mtendaji wa baraza hilo katika jimbo la Michigan ameitaka polisi ya Marekani kuvipa uzito vitisho hivyo. Kadhalika viongozi wa jimbo hilo wameahidi kuchunguza matamshi yoyote yale ya vitisho dhidi ya jamii ya Waislamu eneo hilo. Licha ya kwamba jimbo la Michigan ni eneo wanaopoishi idadi kubwa ya Wauslamu nchini Marekani, lakini bado kumekuwepo fikra ghalati na chuki dhidi ya wafuasi wa dini hiyo. Kwa mujibu wa takwimu za polisi ya Marekani, kiwango cha chuki dhidi ya Waislamu kimeongezeka kwa asilimia 50 baada ya shambulizi la Septemba 11, 2001.

Tags