Nov 23, 2016 04:17 UTC
  • Zaidi ya Misikiti 100 yahujumiwa nchini Uingereza, kuanzia Mei 2013

Zaidi ya ya vituo vya Kiislamu na misikiti 100 imehujumiwa nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya taasisi moja ya kijamii ijulikanayo kama Tell MAMA, ambayo hufuatilia  vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu Uingereza, kuanzia Mei 2013 hadi Septemba mwaka huu, kumekuwepo na hujuma zaidi ya 100 dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu.

Ripoti hiyo imesema aghalabu ya hujuma hizo zinajumuisha uteketezaji moto wa makusudi, kumwaga nyama za nugurwe katika maeneo hayo ya Kiislamu na vitendo vingine vingi vya utumiaji mabavu na vyenye kuwaudhi Waislamu. Kati ya vitendo hivyo ni kuandika maandishi ya chuki dhidi ya Uislamu katika kuta za misikiti.

Waislamu katika Ibada

Hujuma hizo hutekelezwa katika maeneo yenye Waislamu wengi na misikiti kote Uingereza. Aidha imebainika kuwa aghalabu ya hujuma hizo hutekelezwa na makundi yenye misimamo mikali ya mirengo ya kulia.

Mwanzilishi wa Tell MAMA Fiyaz Mughal amesema chuki dhidi ya Waislamu inaelekezwa kwa misikiti ambayo ni nembo ya jamii za Waislamu Uingereza. Aidha amesema misimamo ya kufurutu ada ya makundi ya mrengo wa kulia ni chanzo kikuu cha hujuma hizo.

Tags