-
Ismail Haniya: Muqawama wa Palestina umevuruga mahesabu yote ya adui Mzayuni
Nov 15, 2018 03:31Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: Muqawama wa Palestina umevuruga mahesabu ya adui na kubadilisha mlingano wa nguvu.
-
Hizbullah: Jeshi la anga la Israel haliwezi kuzuia makombora yetu
Sep 13, 2018 02:43Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, imekwishayalenga kwa makombora yake maeneo yote muhimu ya Israel, na kwamba jeshi la anga la utawala huo, halina uwezo wa kuzuia makombora hayo.
-
Silaha ya Muqawama; wenzo wa kuwahami wananchi wa Palestina
Aug 13, 2018 07:30Khalid al-Batsh, kiongozi mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesisitiza kuwa silaha ya Muqawama ndio wenzo wa kulihami taifa na wananchi wa Palestina dhidi ya Wazayuni maghasibu.
-
HAMAS: Shambulio dhidi ya wanamapambano wa Muqawama halitaachwa bila kujibiwa
Aug 08, 2018 04:15Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema shambulio la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza dhidi ya kituo cha brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati hiyo ambalo limesababisha kuuawa shahidi wanamapambano wawili wa Muqawama halitaachwa bila kujibiwa.
-
Waziri wa vita wa Israel atoa vitisho vipya kwa Wapalestina
Jun 05, 2018 03:06Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni ametishia kuwa Israel itamalizia hasira zake kwa harakati za Hamas, Jihadul Islam na makundi yote ya muqawama ya Palestina yanayoendesha mapambano dhidi ya utawala vamizi wa Kizayuni.
-
Hizbullah: Taifa la Palestina litegemee muqawama, lisiwategemee viongozi wa Kiarabu wanafiki
Jun 04, 2018 04:16Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Nabil Qaouk amesisitiza kwamba, taifa la Palestina halitakiwi kuwategemea viongozi wa nchi za Kiarabu na vikao vyao, bali wategemee muqawama na stratijia yake.
-
Israel yahamakishwa na jibu kali lililotolewa na wanamuqawama wa Palestina
May 30, 2018 15:08Jibu kali lililotolewa na muqawama wa Palestina kufuatia jinai za kila mara za askari wa Kizayuni la kuvurumisha makombora 22 kulenga kambi kadhaa za utawala huo, limemkasirisha Waziri wa Sheria wa Utawala Haramu wa Israel na kumfanya atishie kwamba ili kutoa pigo kwa uongozi wa muqawama machaguo yote yako mezani hususan la kuvamia na kulikalia kwa mabavu eneo la Ukanda wa Gaza.
-
Utawala wa Kizayuni wa Israel wahujumu Ukanda wa Ghaza
May 29, 2018 14:06Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel leo zimetekeleza mashambulizi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Velayati: Baada ya muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi ya Muqawama
Apr 20, 2018 04:19Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema: kambi ya muqawama imepanuka kwa kuanzia Iran na kuenea hadi Palestina, Syria na Iraq; na muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi hiyo.
-
Jebeli: Hujuma ya Marekani na Waitifaki wake Syria haiathiri utendaji wa muqawama
Apr 15, 2018 14:10Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Hujuma ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Syria haijawa na taathira hasi katika utendaji wa jeshi na taifa la Syria pamoja na harakati ya mapambano au muqawama."