Hizbullah: Jeshi la anga la Israel haliwezi kuzuia makombora yetu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48100-hizbullah_jeshi_la_anga_la_israel_haliwezi_kuzuia_makombora_yetu
Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, imekwishayalenga kwa makombora yake maeneo yote muhimu ya Israel, na kwamba jeshi la anga la utawala huo, halina uwezo wa kuzuia makombora hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2018 22:13 UTC
  • Hizbullah: Jeshi la anga la Israel haliwezi kuzuia makombora yetu

Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, imekwishayalenga kwa makombora yake maeneo yote muhimu ya Israel, na kwamba jeshi la anga la utawala huo, halina uwezo wa kuzuia makombora hayo.

Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo akihutubia majlisi ya kumbukumbu za mauaji ya mjukuu wa Mtume (saw) Imam Hussein (as) katika viunga vya kusini mwa mji wa Bairut, na kuongeza kuwa, matamshi ya viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni yanaonyesha kwamba, utawala huo khabithi una wasi wasi mkubwa na unatafuta njia mbadala itakayousaidia kutoshindwa tena kama ilivyokuwa huko nyuma. Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kwamba, Wazayuni wanafahamu kwamba, hawana tena uwezo wa kukabiliana na muqawama, kwa kuwa muqawama huo umepiga hatua kubwa na kwamba kwa zana za kijeshi unazozimiliki, unaweza kuendesha vyema shughuli zake.

Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon

Sheikh Naim Qassem ameongeza kwamba, hii leo muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati, umezidi kupanuka kiasi kwamba, taifa la kimapambano la Palestina limesimama imara kukabiliana na Wazayuni na kusisitiza kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwa utawala wa Kizayuni. Kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amefafanua kuwa, Marekani haina uwezo wa kutekeleza mipango yake nchini Iraq na Syria na kwamba hata uwezo wa kutumia vibaraka wake katika Ghuba ya Uajemi kukabiliana na taifa la kimapambano la Yemen.