-
UN: Idadi ya watu ambayo 'haijawahi kushuhudiwa' wanakabiliwa na baa kubwa la njaa Sudan Kusini
Dec 03, 2016 04:17Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa watu wapatao milioni tatu na laki sita wanakabiliwa na uhaba mkubwa mno wa chakula nchini Sudan Kusini ambao ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika msimu wa mavuno, huku hali hiyo ikitazamiwa kuwa mbaya zaidi ifikapo mwakani baada ya chakula cha mavuno ya sasa kumalizika.
-
Indhari ya UN juu ya uwezekano wa kutokea mauaji ya kimbari Sudan Kusini
Dec 02, 2016 13:01Kutokana na kuendelea mapigano nchini Sudan Kusini kuna hatari ya kutokea mauaji ya kimbari nchini humo.
-
UN yatahadharisha kuhusu mauji ya kimbari Sudan Kusini
Dec 02, 2016 00:54Mjumbe wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema baada ya kuitembelea nchi hiyo kuwa, kumetokea mauaji ya kimbari katika maeneo kadhaa ya Sudan Kusini.
-
UN yatiwa wasiwasi na kuongezeka machafuko Sudan Kusini
Dec 01, 2016 03:51Umoja wa Mataifa umesema kuwa una wasiwasi na kushtadi machafuko ya kikabila huko Sudan Kusini.
-
Sudan Kusini ipo tayari kutumwa kikosi kipya cha UN nchini humo
Nov 27, 2016 01:16Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa ipo tayari kuafiki kutumwa nchini humo kikosi kipya cha kudumisha amani wakati wowote, baada ya mapigano ya mwezi Julai huko Juba kutishia kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vikubwa.
-
Rais Salva Kiir atoa amri ya kupambana na vitisho vya waasi
Nov 26, 2016 04:43Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesisitizia udharura wa kukabiliana na vitisho vya makundi ya upinzani vinavyohatarisha usalama wa nchi hiyo.
-
Jeshi la Sudan Kusini lakadhibisha tuhuma za Human Rights Watch
Nov 25, 2016 01:18Jeshi la Sudan Kusini limekadhibisha tuhuma zilizotolewa na shirika la kutetea haki za binaadamu Human Rights Watch juu ya kufanya jinai dhidi ya binaadamu.
-
OCHA: Watu karibu milioni tatu Sudan Kusini wamekuwa wakimbizi tangu 2013
Nov 22, 2016 04:37Ofisi ya uratibu ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinaadamu (OCHA) imeetangaza kuwa, karibu watu milioni tatu raia wa Sudan Kusini wamekuwa wakimbizi wa ndani au katika nchi jirani tangu mwezi Disemba mwaka 2013 hadi sasa.
-
Uchunguzi: Marekani ilishinikiza kutimuliwa kamanda wa Kenya, Sudan Kusini
Nov 20, 2016 04:40Uchunguzi uliofanywa na shirika moja la kimataifa la kutathmini masuala ya sera umefichua kuwa, Marekani ilishinikiza kufutwa kazi kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Kenya aliyekuwa akisimamia Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS).
-
Marekani yataka Machar awekwe katika orodha nyeusi
Nov 19, 2016 00:59Marekani imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limuweka kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar katika orodha nyeusi kwa tuhuma za kupanga njama ya kuipindua serikali ya Rais Salva Kiir.