-
Somalia yakataa ombi la kuangalia upya uamuzi wa kumfukuza mjumbe wa UN
Jan 05, 2019 04:14Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya kufukuzwa nchini Somalia, Nicholas Haysom, mjumbe maalumu wa umoja huo katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika, lakini amesisitiza kuwa nafasi hiyo itajazwa katika siku chache zijazo.
-
Somaliland yalalamikia hatua ya Somalia kumtimua mjumbe wa UN
Jan 03, 2019 23:20Jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland nchini Somalia imekosoa vikali hatua ya serikali ya Mogadishu ambayo Jumanne iliyopita ilimfukuza nchini humo Nicholas Haysom, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa, kutokana na kile ilichokitaja kama mienendo yake mibaya na kuingilia kwake waziwazi mambo ya ndani ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
UNHCR: Vifo vya wahajiri katika Bahari ya Mediterania vimepungua
Jan 03, 2019 11:42Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema wahajiri wapatao 2,262 walifariki dunia katika Bahari ya Mediterania mwaka uliomalizika wa 2018, na kwamba idadi ya wahajiri wanaokufa maji katika safari hizo hatarishi imepungua kwa zaidi ya asilimia 25.
-
Umoja wa Mataifa wataka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji Sudan
Dec 29, 2018 12:53Umoja wa Mataifa umelezea kusikitishwa sana na machafuko pamoja na mauaji ya waandamanaji nchini Sudan na umewataka viongozi wa nchi hiyo wafanye uchunguzi unaotakiwa wa kubaini kwa nini waandamanaji wanauawa.
-
Katibu Mkuu wa UN ataka uchaguzi huru na wa haki Kongo DR
Dec 29, 2018 04:45Huku wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliotimiza masharti ya kupiga kura wakitazamiwa kuelekea katika masanduku ya kupigia kura kumchangua kiongozi atakayerithi mikoba ya Rais Joseph Kabila Jumapili ya kesho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa pande zote husika za kisiasa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa uhuru na amani.
-
Palestina yaomba uanachama wa kudumu katika Umoja wa Mataifa
Dec 26, 2018 22:58Riyad al Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, Rais Mahmoud Abbas wa mamlaka hiyo mwezi ujao wa Januari ataelekea mjini New York Marekani kuwasilisha rasmi ombi la serikali ya Palestina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuwa mwanachama wa kudumu wa umoja huo.
-
Mahmoud Abbas: Trump anapaswa aheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa
Dec 25, 2018 11:18Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameitaka serikali ya Marekani iheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina.
-
UN: Milima ya Golan ni ardhi ya Syria, Wazayuni wanaikalia kwa mabavu
Dec 24, 2018 04:29Kwa mara nyingine tena, Baraza Kuu la Umoja wa Maraifa limepasisha kwa wingi wa kura azimio linalosisitiza kuwa, milima ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel ni ardhi isiyotenganishika na ardhi nyingine za Syria.
-
Bashar al Jaafari: Jamii ya kimataifa iisaidie Damascus kutokomeza ugaidi
Dec 21, 2018 04:48Mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa ameitolea wito jamii ya kimataifa kusaidia kukomesha mashambulizi ya kigaidi nchini kwake.
-
Baraza Kuu la UN lapasisha azimio dhidi ya Marekani
Dec 21, 2018 01:08Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio linaloitaka Marekani kukomesha hatua zilizo kinyume na sheria dhidi ya wawakilishi na maeneo ya kidiplomasia ya Russia nchini humo.