-
UNHCR ina wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu DRC
Oct 17, 2018 15:04Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa, lina wasiwasi na hali ya kibinadamu katika jimbo la Kasai la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na kurejea wakimbizi wengi kutoka Angola katika wiki mbili zilizopita.
-
Watoto wa wakimbizi wanaopotea kiholela waongezeka Ujerumani
Oct 14, 2018 01:11Idadi ya watoto wa wakimbizi wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha inazidi kuongezeka nchini Ujerumani huku idadi ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia nchini humo nayo ikizidi kupungua.
-
Indhari kuhusu safari za wahajiri kuelekea Ulaya zenye kuhatarisha maisha
Sep 03, 2018 13:31Mjumbe Maalumu wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa katika kituo cha Mediterania ametahadharisha kuwa wahajiri hukabiliana na hatari chungu nzima wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania ili kufika Ulaya.
-
Libya yalalamikia vikali jaribio la kurejeshwa wakimbizi nchini humo
Aug 23, 2018 15:06Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amelalamikia juhudi za nchi za Ulaya za kutaka kuwarejesha wakimbizi wa Kiafrika nchini Libya na kusema kuwa jambo hilo ni la kidhalimu, ni kinyume cha sheria na halikubaliki kabisa.
-
Papa aitaka jamii ya kimataifa kukomesha maafa ya wahajiri
Jul 23, 2018 07:54Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameitolea wito jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti za kuzuia kukaririwa maafa ya wahajiri katika maji ya bahari ya Mediterania.
-
Msalaba Mwekundu: Myanmar sio salama kurejea wakimbizi wa Rohingya
Jul 02, 2018 07:40Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema sio salama kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wanaoshi kambini katika nchi jirani ya Bangladesh kurejea makwao katika mkoa wa Rakhine nchini Myanmar.
-
Nchi za kaskazini mwa Afrika zagoma kuwapokea wahajiri wa Kiafrika
Jun 30, 2018 07:31Nchi tano za kaskazini mwa Afrika zimekataa mapendekezo ya viongozi wa Ulaya ya kuanzisha kambi maalumu za wahajiri katika ardhi za nchi hizo kwa ajili ya kuwapokea wahajiri wa Kiafrika.
-
UN: Migogoro yaifanya robo ya wananchi wa CAR kuwa wakimbizi
May 30, 2018 07:52Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema mapigano na migogoro imeifanya asilimia 25 ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.
-
Uganda yaitaka UN iiongezee ufadhili kwa ajili ya wakimbizi
May 06, 2018 07:50Serikali ya Uganda imeutaka Umoja wa Mataifa uongeze msaada na ufadhili wake kwa ajili ya makumi ya maelfu ya wakimbizi walioko nchini humo.
-
Polisi ya Rwanda yawakamata makumi ya wakimbizi wa Kongo DR
May 02, 2018 14:55Polisi ya Rwanda imewatia nguvuni wakimbizi 23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walioko nchini humo, kwa tuhuma za kuwashambulia kwa mawe maafisa waandamizi wa polisi na serikali, waliotembelea kambi yao.