Watoto wa wakimbizi wanaopotea kiholela waongezeka Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48776-watoto_wa_wakimbizi_wanaopotea_kiholela_waongezeka_ujerumani
Idadi ya watoto wa wakimbizi wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha inazidi kuongezeka nchini Ujerumani huku idadi ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia nchini humo nayo ikizidi kupungua.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 14, 2018 01:11 UTC
  • Watoto wa wakimbizi wanaopotea kiholela waongezeka Ujerumani

Idadi ya watoto wa wakimbizi wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha inazidi kuongezeka nchini Ujerumani huku idadi ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia nchini humo nayo ikizidi kupungua.

Shirika la habari la Ujerumani limemnukuu Holger Hoffmann, mkuu wa jumuiya ya ustawi inayojishughulisha na masuala ya watoto wadogo nchini humo akisema kuwa, karibu watoto 900 wa wakimbizi wenye umri wa chini ya miaka 14 hawajulikani walipo hadi hivi sasa. Hii ni katika hali ambayo idadi ya watoto waliopotea katika mazingira ya kutatanisha huko Ujerumani iliongezeka mwezi Oktoba kutoka watoto 895 hadi 902.

Amesema, magenge ya majambazi na wahalifu yanaongezeka mno hivi sasa katika kona zote za Ulaya na yanawarubuni watoto wadogo hasa wenye shida kujiunga nayo na kuwashirikisha katika uhalifu kama wa kijinsia au magendo ya binadamu na ya madawa ya kulevya, au kuwamimina mitaani kuombaomba kwa faida ya magenge hayo.

Image Caption

Hoffmann ameongeza kuwa, hadi hivi sasa hakuna hatua za maana zilizochukuliwa nchini Ujerumani kukabiliana na jambo hilo kutokana na kukosekana taarifa za kutosha juu ya kwa nini watoto hao wanatoweka.

Wimbi la wakimbizi limeongezeka duniani na hasa barani Ulaya kutokana na siasa mbovu na za kibeberu za nchi za Magharibi ambazo zinachochea mapigano kwa kumwaga silaha na kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Mzozo mkubwa uliopo baina ya nchi za Ulaya kuhusu wakimbizi hao ulijitokeza kwa uwazi zaidi katika kikao cha viongozi wa EU cha mwezi Julai mwaka huu wa 2018.