Libya yalalamikia vikali jaribio la kurejeshwa wakimbizi nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47637-libya_yalalamikia_vikali_jaribio_la_kurejeshwa_wakimbizi_nchini_humo
Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amelalamikia juhudi za nchi za Ulaya za kutaka kuwarejesha wakimbizi wa Kiafrika nchini Libya na kusema kuwa jambo hilo ni la kidhalimu, ni kinyume cha sheria na halikubaliki kabisa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 23, 2018 15:06 UTC
  • Libya yalalamikia vikali jaribio la kurejeshwa wakimbizi nchini humo

Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amelalamikia juhudi za nchi za Ulaya za kutaka kuwarejesha wakimbizi wa Kiafrika nchini Libya na kusema kuwa jambo hilo ni la kidhalimu, ni kinyume cha sheria na halikubaliki kabisa.

Shirika la habari la Libya (WAL) limeripoti habari hiyo leo na kumnukuu Mohammad Siala akijibu matamshi ya Matteo Salvini, waziri wa mambo ya ndani wa Italia aliyesema kuwa, karibu wakimbizi 170 wa Kiafrika watarudishwa Libya karibuni hivi na kuongeza kuwa, Libya haiwezi kukubaliana kivyovyote vile na uamuzi huo.

Siala amesema, Libya imegeuzwa kuwa kituo kikuu cha kupitia wakimbizi wa Kiafrika na kwamba wahamiaji haramu wameisababishia hasara kubwa nchi hiyo.

Wakimbizi waliokwamba melini Secilia, Italia baada ya kuokolewa. Serikali ya Rome inataka kuwarudisha Libya

 

Vile vile ameitaka jamii ya kimataifa kuzishinikiza nchi nyingine za Afrika ili zichangie gharama za kuwarejesha nyumbani raia wao wanaoingia Libya kinyume cha sheria.

Hivi karibuni shirika la kimataifa la wahijiri lilisema kuwa, njia ya Libya kuelekea Italia ni kati ya njia za hatari mno zinazotumiwa na wahajiri wa Kiafrika kiasi kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, karibu wahajiri elfu mbili wameshapoteza maisha yao katika njia hiyo.