-
Umri wa unywaji pombe Kenya wapendekezwa kuongezwa kutoka miaka 18 hadi 21
Jul 17, 2025 08:07Mamlaka ya Taifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya nchini Kenya (NACADA) imetetea pendekezo lake la kutaka umri wa kisheria wa kunywa pombe nchini humo uongezwe kutoka miaka 18 hadi 21, ikitaja utafiti wa kiafya, maoni ya umma na viwango vya kimataifa kama msingi wa pendekezo hilo.
-
Dira ya 2050 kuigeuza Tanzania nchi ya Uchumi wa $Trilioni 1
Jul 17, 2025 11:22Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Julai 17 imezindua rasmi Dira ya Taifa ya 2050 katika hafla maalumu iliyohudhuriwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
-
Eswatini kuwatimua wahamiaji 'sugu' kutoka US baada ya malalamiko
Jul 17, 2025 01:29Serikali ya Eswatini ilisema jana Jumatano kwamba, inawashikilia raia watano wa nchi ya tatu waliofukuzwa kutoka Marekani katika magereza yaliyotengwa, chini ya makubaliano na utawala wa Rais Donald Trump, lakini inapania kuwarejesha katika nchi zao.
-
UN: Tuna wasiwasi kutokana na kushtadi mapigano, taharuki Sudan
Jul 16, 2025 09:11Wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa mapigano nchini Sudan, hasa mashambulizi ya karibuni katika Jimbo la Kordofan Kaskazini.
-
Trump kuzisakama nchi maskini za Afrika kwa ushuru wa 10%
Jul 16, 2025 05:15Rais wa Marekani, Donald Trump anapania kupanua ajenda yake ya ushuru, akitangaza mipango ya kutoza ushuru mpya wa forodha wa zaidi ya asilimia 10 kwa bidhaa zinazoagizwa nchini humo kutoka mataifa madogo, ikiwa ni pamoja na kadhaa ya bara Afrika na eneo la Caribbean.
-
Madaktari Wasio na Mipaka: Wafanyakazi wetu waliuawa kwa makusudi Tigray
Jul 16, 2025 04:54Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limesema wafanyakazi wake watatu "waliuawa kwa makusudi" wakati wa mapigano makali katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.
-
Watu 82 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa DAESH watiwa mbaroni Ethiopia
Jul 16, 2025 03:21Shirika la Taifa la Intelijensia la Ethiopia limetangaza kuwa limewakamata watu 82 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS).
-
27 wauawa katika shambulio la watu wenye silaha katika jimbo la Plateau, Nigeria
Jul 15, 2025 13:46Watu wasiopungua 27 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha kaskazini kati mwa jimbo la Nigeria la Plateau, katika machafuko ya hivi karibuni yaliyolikumba eneo hilo ambalo halina usalama wa kutosha.
-
Maelfu wahamishwa baada ya Al-Shabab kudhibiti mji katikati mwa Somalia
Jul 15, 2025 12:52Afisa mmoja wa jeshi la Somalia ametangaza kuwa, wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabab wameuteka mji wa Tardo katika eneo la Hiiran katikati ya nchi hiyo.
-
Wanaharakati Sudan: RSF imeua watu 300 Kordofan Kaskazini
Jul 15, 2025 00:53Wanaharakati wa Sudan wamesema Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kimeua karibu watu 300 katika wimbi jipya la mashambulizi katika jimbo la Kordofan Kaskazini, magharibi mwa nchi.