-
Mwanamke Afrika Kusini afungwa maisha jela kwa kumuuza binti yake
May 30, 2025 04:02Mwanamke mmoja kutoka Afrika Kusini amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumuza binti yake mwenye umri wa miaka sita. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Joshlin Smith, aliuzwa kwa kiasi cha takribani dola 1,122 za Marekani (sawa na R20,000).
-
Milipuko ya kipindupindu yaongezeka Khartoum, Sudan
May 30, 2025 03:48Serikali ya Sudan imetangaza ongezeko kubwa la visa vya kipindupindu katika jimbo la Khartoum, ambapo kwa siku moja tu, visa 1,375 vipya vimeripotiwa, na vifo 23 kuthibitishwa.
-
Rais wa Sudan Kusini amfuta kazi Jaji Mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu
May 29, 2025 23:34Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemfuta kazi Jaji Mkuu wa muda mrefu aliyekuwa pia Mkuu wa Mahakama ya Juu, Chan Reec Madut pamoja na naibu wake John Gatwech Lul.
-
Maafisa wa kijeshi wanaoshirikiana na magaidi watiwa mbaroni Nigeria
May 29, 2025 23:31Jeshi la Nigeria limewatia mbaroni wanajeshi 18, polisi 15 na raia 8 katika operesheni maalumuu ya kupambana na maafisa wa usalama wanaoshirikiana na magenge ya kigaidi ikiwa ni pamoja na kuwapa silaha magaidi hao.
-
Mwandishi maarufu wa Kenya , Ngũgĩ wa Thiong’o, afariki dunia
May 29, 2025 06:25Ngũgĩ wa Thiong’o, gwiji wa fasihi ya Kiafrika na sauti isiyochoka ya ukombozi wa kiakili barani, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 87, familia yake imethibitisha.
-
Jeshi la Marekani latafakari kuondoka Afrika
May 29, 2025 06:20Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM) ametangaza mpango wa kutathmini upya uwepo wa jeshi hilo katika bara la Afrika, huku mataifa mengi yakianza kupima upya ushirikiano wao wa kiulinzi na nchi za Magharibi na kuelekeza ushirikiano wao kwa nchi zingine zisizo za kibeberu.
-
Balozi wa Israel atimuliwa na waungaji mkono Palestina, Senegal
May 29, 2025 02:39Balozi wa Israel nchini Senegal, Yuval Waks, alilazimika kuondoka katika Chuo Kikuu cha Dakar baada ya wanafunzi kupinga uwepo wake na kupiga nara za kuunga mkono Palestina chuoni hapa.
-
Namibia yataka fidia ya 'maana' ya mauaji ya halaiki ya Ujerumani
May 29, 2025 02:31Namibia imefanya kumbukizi ya kuwaenzi wahanga wa mauaji ya kibari wakati wa utawala wa kikoloni wa Ujerumani, huku viongozi, wanasiasa na wakuu wa jamii zilizoathirika na ukatili huo wa askari wa Kijerumani wakitoa wito mpya wa kulipwa fidia na Berlin.
-
Waafrika wazidi kuonesha ubinadamu, wampa tunzo maalumu Yahya Sinwar
May 28, 2025 07:17Waafrika kwa mara nyingine wameonesha hisia zao za kuthamini ubinadamu kwa kuenzi nafasi muhimu ya wanamapambano wa Palestina. Tuzo ya ya kila mwaka ya "Kwame Tour" kwa mwaka huu 2025 amepewa kiongozi wa Palestina shujaa shahid Yahya Sinwar (Abu Ibrahim) wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Afrika.
-
Mgogoro wa kibinadamu Sudan unazidi kuongezeka, mapigano yanaendelea
May 28, 2025 07:16Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan unazidi kuongezeka huku mapigano yakiendelea, watu wanazidi kuhama makazi yao na udharura wa kuchukuliwa hatua za kiafya umezidi kuwa mkubwa.