-
Ramaphosa: Hujuma dhidi ya wageni haziakisi maoni ya Afrika Kusini
May 12, 2026 04:04Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa "wahalifu walipanga mashambulizi dhidi ya wageni na kuzitoa hofu nchi nyingine za Afrika, ambazo zimeelezea wasiwasi wao kuhusu raia wake waliopo Afrika Kusini.
-
Zambia yapinga matakwa ya Marekani yanayohusiana na mkataba wa afya na madini
May 10, 2026 10:24Zambia imeishutumu hadharani Marekani kwa kuunganisha kifurushi cha afya kilichopendekezwa cha dola bilioni 2 na matakwa kupewa data na madini na muhimu, ikisema baadhi ya masharti yaliyoambatanishwa na makubaliano hayo "hayakubaliki".
-
Wananchi wa Mali waandamana kumuunga mkono kiongozi wao wa kijeshi
May 10, 2026 10:09Mamia ya waungaji mkono wa uongozi wa serikali ya kijeshi ya Mali Jumamosi walijumuika katika uwanja wa michezo katika mji mkuu, Bamako ili kuthibitisha uungaji mkono wao kwa serikali ya mpito ya nchi hiyo.
-
Niger yasimamisha vyombo tisa vya habari vya Ufaransa
May 10, 2026 09:28Serikali ya Niger imetangaza kusimamisha shughuli za vyombo tisa vya habari vya Ufaransa, ikieleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na “usambazaji wa mara kwa mara wa maudhui yanayoweza kuhatarisha kwa kiasi kikubwa utulivu wa umma, umoja wa taifa, mshikamano wa kijamii, na uthabiti wa taasisi za Jamhuri.”
-
Watu 70 wauawa kaskazini mashariki mwa Kongo; Umoja wa Mataifa walaani ghasia
May 10, 2026 07:37Kwa uchache watu 70, wengi wao wakiwa raia, wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha waliohusishwa na wanamgambo wa CODECO, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wapinzani Afrika Kusini waapa kumuondoa madarakani Ramaphosa
May 09, 2026 09:54Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) nchini Afrika Kusini, amemtaka Rais Cyril Ramaphosa wa nchi hiyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo na taratibu za kumfungulia mashtaka zianze.
-
Burundi kufanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao
May 09, 2026 09:47Burundi itafanya uchaguzi wa rais Mei 3 mwaka ujao. Habari hiyo ilitangazwa Ijumaa na Tume ya Uchaguzi, wakati wa mkutano uliosusiwa na upinzani.
-
Rais Tshisekedi asema huenda akagombea muhula wa tatu wa urais, Kongo
May 07, 2026 11:13Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amezungumzia uwezekano wa kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu, akisema atakubali kuendelea kuiongoza nchi hiyo iwapo ataungwa mkono na Wakongo kupitia kura ya maoni.
-
Rais wa Sudan Kusini awafuta kazi Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Fedha
May 07, 2026 10:50Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewafukuza kazi Mkuu wa Jeshi na Waziri wa Fedha. Waziri wa Fedha alikuwa amehudumu katika wadhifa huo chini ya wiki mbili.
-
Boko Haram yauwa wanajeshi 23 katika eneo la Ziwa Chad
May 06, 2026 10:49Takriban wanajeshi 23 wa Chad wameuawa na 26 kujeruhiwa katika shambulio la wanamgambo wa Boko Haram kwenye kituo cha kijeshi katika eneo la Ziwa Chad.