-
Ufaransa yashutumiwa kupanga kuangusha serikali pinzani barani Afrika
Feb 02, 2026 22:58Ufaransa inapanga “mapinduzi ya kikoloni mamboleo” katika mataifa mbalimbali ya Afrika kwa lengo la kuangusha serikali inazoziona kuwa “zisizohitajika,” hususan katika eneo la Sahel ambako imepata pigo kubwa katika miaka ya hivi karibuni. Shirika la Ujasusi wa Kigeni la Urusi (SVR) limedai.
-
Wanajeshi wa Nigeria wamuua kamanda wa kundi la kigaidi la Boko Haram
Feb 02, 2026 10:26Jeshi la Nigeria limetangaza Jumapili kuwa vikosi vyake vimemuua kamanda mmoja wa kundi la kigaidi la Boko Haram pamoja na magaidi wengine 10 waliokuwa naye katika operesheni iliyofanyika kaskazini mashariki mwa nchi.
-
Umoja wa Mataifa: Tuna wasiwasi kuhusu kuongezeka vurugu na machafuko Sudan Kusini
Feb 02, 2026 03:41Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika taarifa kwamba ana wasiwasi mkubwa kuhusu athari za kuongezeka vurugu na machafuko nchini Sudan Kusini, akiongeza kuwa hali hii itawadhuru zaidi raia ambao tayari wako katika hali hatarishi.
-
Mazungumzo ya kitaifa DRC: Masharti ya Rais Tshisekedi yaibua hisia mseto
Feb 02, 2026 03:40Siku moja baada ya mfumo uliowekwa na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa yaliyoitishwa na sehemu ya upinzani na kuhimizwa na washirika kadhaa wa Magharibi wa DRC kutatua mgogoro unaosambaratisha mashariki mwa nchi, wengi mjini Kinshasa wametoa hisia zao.
-
Hali ya Tigray nchini Ethiopia yamtia wasiwasi mkubwa Katibu Mkuu wa UN
Feb 01, 2026 23:38Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anafuatilia kwa karibu kinachoendelea katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, ambako mvutano unaoibuka upya na taarifa za mapigano vimechangia kuzorota kwa hali ya usalama.
-
Afrika Kusini yamtimua Kaimu Balozi wa Israel
Feb 01, 2026 23:11Afrika Kusini imemtangaza kaimu balozi wa utawala wa Isarel nchini humo kuwa mtu asiyehitajika na kuamuru aondoke mara moja.
-
Umoja wa Afrika walaani mashambulizi dhidi ya Niger; waahidi kuiunga mkono nchi hiyo
Feb 01, 2026 03:34Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf amelaani mashambulizi ya hivi karibuni huko Niger ikiwa ni pamoja na shambulio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamani Diori katika mji mkuu Niamey. Ali Youssouf amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba Umoja wa Afrika uko pamoja na Niger.
-
Malawi yatangaza mlipuko wa polio baada ya kugundua sampuli za ugonjwa huo
Feb 01, 2026 03:33Serikali ya Malawi imetangaza kuibuka virusi vya polio aina ya 2 (cVDPV2) kufuatia kugunduliwa kwa sampuli za mazingira.
-
Kipindupindu chauwa watu 12 Msumbiji huku kesi za ugonjwa huo zikiongezeka Malawi
Jan 31, 2026 23:22Msumbiji imesajili vifo vya watu 12 kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika muda wa saa 24 zilizopita pamoja na kesi mpya za ugonjwa huo 135. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana Jumamosi.
-
Zaidi ya watu 200 wamefariki DRC kwa maporomoko kwenye mgodi unaodhibitiwa na waasi
Jan 31, 2026 23:00Watu wasiopungua 200 wameaga dunia mapema wiki hii wakati mvua kubwa iliposababisha mfululizo wa maporomoko ya udongo katika mgodi wa madini ya koltani ulioko Rubaya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, eneo ambalo tangu mwaka 2024 liko chini ya udhibiti wa kundi la waasi la M23.