El Baradei awashambulia watawala wa Kiarabu vibaraka wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137756-el_baradei_awashambulia_watawala_wa_kiarabu_vibaraka_wa_marekani
Mwanasiasa mashuhuri wa Misri amekosoa utiifu wa baadhi ya watawala wa Kiarabu vibaraka wa Marekani na uungaji mkono wao kwa Washington kwenye vita vyake dhidi ya Iran.
(last modified 2026-04-03T04:40:13+00:00 )
Apr 03, 2026 04:40 UTC
  • Mohamed El Baradei, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa IAEA
    Mohamed El Baradei, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa IAEA

Mwanasiasa mashuhuri wa Misri amekosoa utiifu wa baadhi ya watawala wa Kiarabu vibaraka wa Marekani na uungaji mkono wao kwa Washington kwenye vita vyake dhidi ya Iran.

Mohamed El Baradei, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na mwanasiasa maarufu wa Misri, amekosoa vikali ubarakala wa watawala wa Kiarabu kwa Marekani na uungaji mkono wao kwa vita dhidi ya Iran.

El Baradei, amepinga uwepo wa wanajeshi wa kigaidi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi kwa kisingizio cha kuhakikisha usalama wa nchi za Kiarabu na matokeo mabaya ya uwepo huo kwa nchi hizo, na kuwaambia watawala wa Kiarabu waliosalimu amri kwa Marekani kwamba: Wakati utawala wa Trump umewauza washirika wake wa karibu wa Ulaya katika shirika la NATO kwa sababu tu wamekataa kujiunga na vita vyake vya kichokozi dhidi ya Iran, je, mtu huyu ndiye tunayepaswa kumtegemea kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa eneo letu la Kiarabu na kulinda haki na maslahi yetu?

Wakati huo huo, Bloomberg News pia imeandika kuwa, vyanzo vya habari vinasema kadiri vita dhidi ya Iran vinavyoendelea, mataifa ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi yanazidi kukatishwa tamaa na Marekani. Mataifa hayo yanahoji faraghani dhamana za usalama za Marekani na kuelezea wasiwasi wao kuhusu kutokuwepo mkakati uliowazi katika utawala wa Trump.

Bloomberg News imeripoti kuwa maafisa wengi wa nchi za Kiarabu wanatilia shaka mantiki ya Trump, kiwango cha kujitolea, na malengo ya vita vyake dhidi ya Iran. Kwa mujibu wa vyanzo ambavyo havikutaka kutajwa majina, nchi za Kiarabu zinatilia shaka hata thamani ya kuwa mwenyeji wa kambi za jeshi la Marekani ambazo sasa zimezifanya nchi hizo kuwa shabaha ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran.