Mufti Mkuu wa Libya awataka Waislamu kuinga mkono Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137540-mufti_mkuu_wa_libya_awataka_waislamu_kuinga_mkono_iran
Mufti Mkuu wa Libya ametoa taarifa kuhusu mashambulizi na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran akisisitiza kuwa: Ni wajibu kuwahami Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.
(last modified 2026-03-23T07:11:03+00:00 )
Mar 23, 2026 07:11 UTC
  • Sheikh Sadiq al Ghariani
    Sheikh Sadiq al Ghariani

Mufti Mkuu wa Libya ametoa taarifa kuhusu mashambulizi na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran akisisitiza kuwa: Ni wajibu kuwahami Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.

Sheikh Sadiq al Ghariani amesema katika taarifa yake iliyoakisiwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba: “Katika Qur’ani Tukufu hakuna kitu kinachoitwa kutopendelea upande wowote. Ni wajibu kuwahami na kuwatetea Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.”

Mufti Mkuu wa Libya anaendelea kusema: Mtu yeyote ambaye inapotokea vita baina ya Waislamu na makafiri huutaja msimamo wake kuwa ni wa “kutopendelea upande wowote” huwa miongoni mwa wale Qur’ani inasema ni vizabazabina baina ya huku na kule. Huku hawako na kule hawako.

Sheikh Al Ghariani amesema: “Miongoni mwa masomo na darsa zinazoona katika vita vya sasa ni kwamba Mustakbirina (mabeberu) wanapaswa kulipa gharama zake, bila kujali wana nguvu kiasi. Hii leo, Rais wa Marekani ameziomba nchi zote duniani zisaidie kufungua Lango Bahari la Hormoz na amepoteza matumaini.”    

Mufti Mkuu wa Libya amewahutubu Waislamu akisema: Acheni wajifunze kutokana na yale yanayojiri katika kambi za kijeshi za Marekani huko Ghuba ya Uajemi; uwepo wao umekuwa sababu ya kushambuliwa nchi walizokuwa wakidhani kwamba wanazilinda. Mtu yeyote anayekata izza na utukufu, basi utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini.”