-
Jeshi la Sudan lakanusha madai ya RSF ya kuteka makao makuu ya jimbo la Sennar
Jun 30, 2024 22:52Jeshi la Sudan (SAF) jana Jumapili lilikanusha madai kwamba Askari wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wamechukua udhibiti wa mji wa Singa ambao ni makao makuu ya jimbo la Sennar la katikati mwa Sudan.
-
Nchi za Afrika zahimizwa kuharakisha utekelezaji wa AfCFTA
Jun 30, 2024 22:51Nchi za Afrika zimetakiwa kuwasilisha mipango ya utekelezaji na mikakati ya kitaifa ili kuharakisha ufanikishaji wa malengo ya kuanzishwa Eneo Huria la Biashara ya Bara la Afrika (AfCFTA) na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za bara hilo.
-
Watu 18 wauawa katika mashambulizi ya kigaidi jimboni Borno, Nigeria
Jun 30, 2024 07:55Kwa akali watu 18 wamepoteza maisha huku makumi ya wengine wakijeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Ghazouani aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais Mauritania
Jun 30, 2024 03:26Rais Mohamed Ould Cheikh Ghazouani wa Mauritania yupo kifua mbele huku ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana Jumamosi ukiendelea.
-
Human Rights Watch: Waliouawa katika maandamano ya Kenya wanakaribia 30
Jun 29, 2024 22:46Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, karibu watu 30 wameaga dunia katika maandamano ya wiki hii ya kupinga muswada wa fedha wa 2024 ambao unaongeza ushiru wa bidhaa.
-
Mji wa Kanyabayonga DRC watekwa na waasi wa M23
Jun 29, 2024 22:45Mji wa kimkakati wa Kanyabayonga, wa kaskazini mwa mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umetekwa na waasi wa M23.
-
Jeshi la Nigeria laangamiza magaidi 2,245 ndani ya miezi 3
Jun 29, 2024 08:49Mkurugenzi wa shughuli za vyombo vya habari vya jeshi la Nigeria, Meja Jenerali Edward Buba amesema kuwa watu 1,993 waliokuwa wametekwa nyara wameokolewa baada ya wahalifu kupewa kikomboleo huku, silaha 2,783 za magaidi zikinaswa.
-
Al-Burhan kumtangaza waziri mkuu mpya wa Sudan
Jun 29, 2024 03:50Mkuu wa Baraza la Utawala na Kamanda wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, anakaribia kumtangaza waziri mkuu mpya atakayeunda serikali ya kitaifa.
-
Ennahda Tunisia yalaani kuendelea kufungwa Rached Ghannouchi
Jun 29, 2024 02:57Harakati ya Ennahda ya Tunisia jana Ijumaa ililaani kifungo cha kiongozi wake, Rached Ghannouchi, kutozwa faini, na kuwekwa chini ya udhibiti wa kiutawala kwa miaka 3.
-
UN: Maelfu ya watu Sudan Kusini wanakabiliwa na janga la uhaba wa chakula
Jun 28, 2024 22:46Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, Sudan Kusini inakabiliwa na janga la ghasia, mafuriko, mgogoro wa kiuchumi na njaa, huku watu 79,000 katika Jimbo la Jonglei pekee wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.