-
Mbunge akamatwa kwa "uchochezi" kuhusu ajali ya ndege nchini Malawi
Jun 22, 2024 23:15Polisi nchini Malawi wamemkamata Mbunge, Kamlepo Kalua, na mwanaharakati, Bon Kalindo, kutokana na maneno waliyoandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali ya ndege iliyotokea Juni 10 iliyoua Makamu wa Rais wa nchi hiyo Saulos Chilima na maafisa wengine wanane.
-
Rais wa Tunisia amfuta kazi waziri kwa vifo vya makumi ya Mahujaji Makka
Jun 22, 2024 07:48Rais Kais Saied wa Tunisia amempiga kalamu nyekundu Waziri wa Masuala ya Dini wa nchi hiyo, Brahim Chaibi, akimbebesha dhima ya vifo vya makumi wa raia wa nchi hiyo, waliokuwa miongoni mwa malaki ya Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Allah mjini Makka, Saudi Arabia mwaka huu.
-
Mudavadi: Kuweka kando Muswada wa Fedha ni sawa na kuangusha Serikali ya Kenya
Jun 22, 2024 03:19Kinara wa Mawaziri wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema Muswada wa Fedha 2024 lazima upitishwe na kutiwa saini na Rais William Ruto kuwa sheria, akisema kinyume na hivyo itakuwa ni sawa na kuangusha Serikali.
-
Kagame: Sijawahi kuweka masharti ya kukutana na Félix Tshisekedi
Jun 22, 2024 00:53Rais Paul Kagame wa Rwanda amezungumzia uhusiano uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao umezorota katika siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka mivutano.
-
Hali ya wakimbizi barani Afrika ni mbaya
Jun 22, 2024 00:35Hali ya wakimbizi barani Afrika inaelezwa kuwa mbaya huku idadi ya wakimbizi ikiripotiwa kuongezeka kila siku katika mataifa mbalimbali ya bara hilo.
-
RSF yatangaza kuteka mji muhimu na wa kimkakati wa kusini mwa Sudan
Jun 21, 2024 22:53Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kimetangaza kwamba kimeuteka kikamilifu mji muhimu na wa kimkakati wa el-Fula ambao ni makao makuu ya Jimbo la Kordofan Magharibi kutokana mikononi mwa jeshi la Sudan.
-
Afrika yahimizwa kutumia mno teknolojia ya AI kuharakisha ustawi na maendeleo
Jun 21, 2024 22:52Bara la Afrika limehimizwa kutumia fursa zinazopatikana kwenye teknolojia ya Akili Mnemba au Artificial Inteligence (AI) kwa kimombo ili kustawisha uchumi na kuongeza idadi na ufanisi kwa wafanyakazi wake.
-
Michael Usi ateuliwa kuwa Makamu mpya wa Rais Malawi baada ya kifo cha Saulos Chilima
Jun 21, 2024 09:07Rais Lazarus Chakwera wa Malawi amemteua Michael Usi kuwa makamu mpya wa rais wa nchi hiyo kuchukua nafasi ya Saulos Chilima aliyefariki katika ajali ya ndege tarehe 10 mwezi huu wa Juni.
-
WFP: Msaada wa chakula waongezeka Darfur lakini hautoshi
Jun 21, 2024 08:48Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema kuwa, jimbo la Darfur limeshuhudia ongezeko la msaada wa chakula unaohitajika, lakini likaonya kwamba kiwango hicho bado hakitoshi kuzuia baa la njaa.
-
Umoja wa Afrika kuchunguza ombi kuhusu wanajeshi wa ATMIS Somalia
Jun 21, 2024 08:26Umoja wa Afrika (AU) umesema kuwa, unalichunguza ombi la Somalia la kupunguza kasi ya kuondoka vikosi vya kulinda amani vya umoja huo (ATMIS) vyenye jukumu la kupambana na kundi al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaida.