-
Waziri Mkuu wa Malaysia aonya kuongezeka uingiliaji wa kigeni nchini Sudan
Nov 22, 2025 03:44Waziri Mkuu wa Malaysia ameonya kuhusiana na kuongezeka kwa uingiliaji wa kigeni nchini Sudan.
-
Afrika Kusini yasema haitakabidhi kwa balozi mdogo wa Marekani urais wa G20 wa 2026
Nov 21, 2025 23:57Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Vincent Magwenya amesema, kiongozi huyo hatomkabidhi balozi mdogo wa Marekani urais wa mkutano wa G20 kwa mwaka 2026 baada ya Marekani kusisitiza kuwa haitohudhuria mkutano huo rasmi jijini Johannesburg.
-
Mahakama ya Nigeria yamhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa Wabiafra wanaopigania kujitenga
Nov 21, 2025 23:11Mahakama ya Nigeria imemhukumu Nnamdi Kanu, kiongozi wa harakati ya kupigania kujitenga ya Watu wa Asili wa Biafra (IPOB), kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na hatia ya mashtaka yote saba aliyoshtakiwa yanayohusiana na ugaidi.
-
Harakati ya M-23: Mazungumzo ya amani na serikali ya Congo yanaendelea
Nov 21, 2025 07:00Harakati ya M-23 imethibitisha kwamba mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Doha yataendelea katika wiki zijazo.
-
Vyama vipya 25 vyasajiliwa, 30 vikiwasilisha maombi ya kusajiliwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Kenya
Nov 21, 2025 06:26Karibu vyama vipya 25 vya kisiasa vimepata usajili wa muda katika kipindi cha miezi michache iliyopita nchini Kenya, huku vingine zaidi ya 30 vikiwasilisha maombi ya kusajiliwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
-
Waasi wa RSF wameharibi viwanda zaidi ya 1,800 huko Khartoum, Sudan
Nov 21, 2025 04:29Waziri wa Viwanda na Biashara wa Sudan, Mahasen Ali Yaqoub, amesema kuwa zaidi ya viwanda 1,800 vimeharibiwa na kundi la waasi wa Rapid Support Forces (RSF) katika jimbo la Khartoum.
-
Rais wa Afrika Kusini akiashiria ubabe wa Marekani asema, hakuna taifa linalopaswa kulitisha jingine
Nov 21, 2025 04:28Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa hakuna taifa linalopaswa kulitisha jingine kwa nguvu za kiuchumi au kijeshi, akieleza kuwa mataifa yote ni sawa. Kauli hiyo ya kupinga ubabe wa Marekani imetolewa mjini Boksburg, mashariki mwa Johannesburg, wakati wa hitimisho la mkutano wa kijamii wa G20.
-
Makubaliano ya dola bilioni 1.4 ya kufufua reli ya TAZARA
Nov 21, 2025 04:27China, Zambia na Tanzania zimesaini makubaliano ya kihistoria ya dola bilioni 1.4 siku ya Alhamisi ya kufufua reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
-
WFP: Karibu robo ya wananchi wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali
Nov 20, 2025 23:32Mpango wa Chakula Duniani (WFP) jana ulitahadharisha kuwa karibu robo ya jamii ya watu wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali huku watoto zaidi ya milioni 1.85 walio na umri chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari ya kupata utapiamlo mkali.
-
Nigeria yafunga shule katika jimbo la Kwara kufuatia ongezeko la ukosefu wa usalama
Nov 20, 2025 23:31Mamlaka husika katika Jimbo la Kwara nchini Nigeria zimefunga shule zote katika eneo la Iflodun, Ekiti, Irepodun, Isin na Oke Ero kufuatia vitisho vipya vya usalama katika jimbo hilo.