-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mapenzi makubwa ya wananchi kwa shahidi Raisi ulikuwa ujumbe kwa dunia kwa manufaa ya Iran
May 24, 2024 13:04Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema amemtaja Rais shahidi wa Iran kuwa ni dhihirisho la nara za Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Mapenzi waliyoonyesha wananchi kwake yametoa ujumbe kwa walimwengu kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Mahudhurio makubwa ya wananchi katika mazishi ya mashahidi wahudumu wa nchi yalikuwa ni utiifu kwa mfumo wa Kiislamu
May 24, 2024 10:50Khatibu wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran amesema kuwa ujumbe wa mahudhurio makubwa ya wananchi katika mazishi ya mashahidi wahudumu wa wananchi katika miji mbalimbali ya Iran ni dhihirisho la utiifu wa wananchi kwa mfumo wa Kiislamu, kutoa shukran zao kwa wahudumu wa taifa hili, kudhihirisha umoja na mshikamano, mafanikio ya diplomasia ya Iran na uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Jeshi la Iran latoa ripoti ya awali kuhusu ajali ya helikopta iliyopelekea kufa shahidi Raisi
May 24, 2024 04:18Kamandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uchunguzi wao wa awali umebaini kuwa, hakuna kitu chochote kisichokuwa cha kawaida kinachoweza kuhusishwa na ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini magharibi mwa nchi.
-
Makamanda wa IRGC na wakuu wa kambi ya muqawama wakutana Tehran
May 24, 2024 03:56Makamanda waandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wamekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya muqawama waliokuja hapa nchini Iran kushiriki mazishi ya viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu akiwemo Rais Ebrahim Raisi waliokufa shahidi katika ajali ya helikopta Jumapili iliyopita.
-
Balozi Saffar: Iran na Uganda kuendeleza uhusiano wao mzuri baina yao
May 23, 2024 23:09Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Kampala Uganda amesema kuwa, kifo cha Rais Ebrahim Raisi hakitaathiri uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
-
Ali Bagheri Kani: Muqawama umewadhalilisha Wazayuni katika uga wa diplomasia
May 23, 2024 23:08Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Iran amesema kuwa, muqawama umewadhalilisha Wazayuni katika uga wa kidipolasia.
-
Watu milioni 3 washiriki mazishi ya Rais Ebrahim Raisi mjini Mashhad
May 23, 2024 10:14Waombolezaji zaidi ya milioni tatu wameshiriki katika mazishi ya kumuaga na Rais Ebrahim Raisi wa Iran, aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita katika mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini magharibi mwa Iran.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran azikwa mjini Rey, mkoani Tehran
May 23, 2024 09:02Mwili wa Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita kaskazini magharibi mwa nchi umezikwa leo katika Haram ya Shah Abdol-Azim katika mji wa Shahre-Rey, kusini mwa Tehran.
-
Kaimu Rais: Iran itaendelea kuunga mkono kambi ya muqawama
May 23, 2024 07:32Kaimu Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono kikamilifu kambi ya muqawama.
-
Mahudhurio makubwa ya kuwaaga Mashahidi Wahudumu wa Iran
May 23, 2024 06:16Mahudhurio makubwa ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hafla ya mazishi ya shahidi Ebrahim Raisi na wenzake ambao walikufa shahidi katika ajali ya helikopta katika eneo la milimani la mkoa wa Azarbaijan Mashariki, kaskazini-magharibi mwa Iran kwa mara nyingine tena yamedhihirisha mshikamano na umoja wa taifa la Iran na nia yao ya kuendeleza njia ya mapambano na muqawama.