May 24, 2024 02:38 UTC
  • Ali Bagheri Kani: Muqawama umewadhalilisha Wazayuni katika uga wa diplomasia

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Iran amesema kuwa, muqawama umewadhalilisha Wazayuni katika uga wa kidipolasia.

Ali Bagheri Kani, amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya muqawama waliokuja hapa nchini kushiriki mazishi ya viiongozi wa Iran akiwemo Ebrahim Raisi waliokufa shahidi katiika ajali ya helikopta.

Bagheri Kani sambamba na kuthamani hatua ya viongozi hao ya kuonyesha kuwa pamoja taifa la Iiran katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kitaifa amebainisha kwamba, muqawama ni malengo yaliyojengeka juu ya vielezo vya ukweli na ndio maana katika makabiliano yake ya miezi saba na nusu na wavamizi ni taifa la Palestina ndilo ambalo limetundika juu bendera ya heshima, izza na mamlaka ya kujitawala.

Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran akizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya muqawama

 

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran ameashiria utendaji na juhudi za kimsingi za Ebrahim Raisi na Hussein Amir Abdollahian katika kuunga mkono haki halali za wananchi wa Palestina na muqawama na kueleza bayana kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafanya kila iwezalo katika kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina na mapambano halali ya muqawama dhidi ya Wazayuni na kukomeshwa jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.

Tags