-
Mkuu wa jeshi la Pakistan azungumza kwa kina na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Tehran
May 23, 2026 12:35Asim Munir, Mkuu wa jeshi la Pakistan amefanya mazungumzo ya muda mrefu na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araqchi mjini Tehran, huku jitihada za kidiplomasia zikishika kasi ili kuzuia kushtadi hali ya mgogoro katika Asia Magharibi.
-
Iran yaiambia UN: Nchi za Ghuba ya Uajemi zinapasa kutoa jibu na kulipa fidia kwa mchango wao katika vita vya Marekani na Israel
May 23, 2026 12:32Amir Saeid Iravani Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi na Jordan zinabeba dhima ya kuzisaidia Marekani na Israel katika uvamizi wao dhidi ya Iran.
-
Kamanda Talaei-Nik: Trump hana chaguo ila kukubali haki ya Iran
May 23, 2026 12:29Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran amesema: "Kushindwa adui kufungamana na matakwa halali ya taifa la Iran kutasababisha gharama kubwa na kushindwa zaidi adui Mzayuni na Marekani."
-
Rais Pezeshkian awataka wataalamu wa mahusiano ya umma kuvunja vikwazo vya vyombo vya habari vya Kizayuni
May 23, 2026 03:05Rais Masoud Pezeshkian anasema wataalamu wa mahusiano ya umma wanapaswa kuchukua jukumu muhimu katika kuongeza uelewa wa umma, ikizingatiwa kwamba vyombo vya habari vya Kizayuni vinawazuia watu kuona na kujua ukweli.
-
Baqaei: Kuharibiwa Taasisi ya Pasteur ya Iran ni tishio kwa usalama wa afya wa kikanda
May 23, 2026 02:41Ismail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amechapisha nukuu ya ripoti ya jarida la masuala ya tiba la The Lancet kuhusu uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Taasisi ya Pasteur ya Iran, na kusisitiza kwamba kuharibiwa taasisi hiyo ni tishio kwa usalama wa kikanda.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa Tehran: Maadui watakabiliana na makombora mapya ikiwa watafanya makosa
May 22, 2026 15:05Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Iwapo maadui watafanya kosa jingine, watakabiliana na vita vipana zaidi badala ya vita vya kikanda, na badala ya kuzuiliwa Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati huo Mlango Bahari wa Bab al-Mandeb pia atafungwa.
-
Pezeshkian: Serikali imejitolea kikamilifu kuboresha uwezo wa Jeshi la Iran
May 22, 2026 06:55Rais Masoud Pezeshkian amesema serikali yake itatumia “nguvu na rasilimali zote zilizopo” kuimarisha majeshi ya ulinzi huku akisifu majibu ya kijeshi ya Iran kuwa “makini, madhubuti na yanayozuia uchokozi” kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na tawala za Marekani na Israel.
-
Jenerali Qa'ani: Freedom Flotilla imewafedhehesha Wazayuni
May 22, 2026 04:29Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema katika ujumbe wake kwamba mafanikio ya msafara wa meli za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ukanda wa Gaza "Global Sumud Flotilla, yanaendelea.
-
“Tutawafanya maadui wajute”: Qalibaf aonya dhidi ya njama za Marekani kuanzisha vita vipya
May 21, 2026 13:24Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa onyo kali akisema kuwa mienendo ya wazi na ya siri ya adui inaashiria wazi kuwa wanapanga kuanzisha duru nyingine ya vita.
-
Kiongozi Muadhamu amkumbuka Shahidi Rais Raeisi, ampongeza kwa uwajibikaji
May 21, 2026 04:42Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa ujumbe wa kuadhimisha mwaka wa pili tangu kufa shahidi aliyekuwa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ebrahim Raeisi. Katika ujumbe huo, alimwelezea marehemu Rais Raeisi kama kiongozi aliyekuwa na hisia ya juu ya uwajibikaji, mwenye kuzingatia uadilifu, mwenye kuendesha diplomasia hai na yenye manufaa, na hasa aliyekuwa karibu na wananchi kwa unyenyekevu na huruma.