Seneta wa Marekani akiri: Hatutafikia malengo yetu yoyote katika vita na Iran
Chris Murphy, Seneta wa chama cha Democrat nchini Marekani, kufuatia kikao cha faragha na maafisa wa utawala wa Rais Donald Trump kuhusu uvamizi wa kijeshi dhidi ya Iran, amekosoa mtazamo wa utawala huo na kusema: "Hatutafikia malengo yoyote tuliyotangaza katika vita dhidi ya Iran."
Amesema: "Imethibitika wazi kwamba vita hivi ni vya kuchanganyikiwa kabisa maasifa wa serikali na wala havina mipangilio inayofaa. Amesema ni dhahiri kwamba utawala wa Trump hautafikia malengo yoyote yaliyotangazwa rasmi. Tayari tulijua kuwa mashambulizi ya anga ya Marekani hayataweza kuharibu mipango ya nyuklia ya Iran."
Seneta huyo wa Connecticut ameendelea kusema: "Utawala wa Trump umethibitisha kwamba 'mabadiliko ya serikali' hayamo katika mipango pia. Kwa hivyo, mamia ya mabilioni ya dola za kodi ya Wamarekani zitatumika na Wamarekani wengi watauawa."
Wanadai kuharibu makombora mengi, meli na viwanda vya ndege zisizo na rubani, lakini swali gumu hapa ni, je, nini kitafanyika baada ya ulipuaji wa mabomu kusimama, na uzalishaji wa maombora na ndege hizo kuanza tena? Kuhusiana na kufungwa kwa Lango-Bahari la Hormuz na Iran, Seneta huyo wa Democrat amesema: "Hivi sasa, serikali ya Marekani imechanganyikiwa isijue itakavyolifungua tena."