-
Iran: Kutumiwa kisiasa IAEA kutatufanya tutoe jibu tofauti
Sep 06, 2021 02:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameionya vikali Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) dhidi ya kufanya mahesabu ghalati katika mkutano wake ujao na kusisitiza kuwa, kutumiwa kama jukwaa la kisiasa taasisi hiyo kutailazimisha Tehran itoe jibu tofauti.
-
Qalibaf: Kuondoka kwa madhila Afghanistan, dalili ya kusambaratika US
Sep 05, 2021 22:34Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema hatua ya Marekani kuondoka kwa fedheha na madhila nchini Afghanistan imeonesha wazi kuwa Washington iko katika mkondo wa kusambaratika na kupoteza nguvu na ushawishi wake katika uga wa kimataifa.
-
Iran yaanza awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo ya Razi Cov Pars ya COVID-19
Sep 05, 2021 06:26Iran imeanzisha awamu ya tatu ya majaribio ya mwanadamu ya chanjo yake ya pili ya COVID-19 inayojulikana kama Razi Cov Pars.
-
Raisi: Usalama na amani ya nchi jirani ni usalama wa Iran
Sep 05, 2021 02:50Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran usiku wa kuamkia leo na katika mazungumzo yake ya kwanza mubashara na wananchi kupitia televisheni ya taifa amesema Jamhuri ya Kiislamu inatambua amani na usalama wa nchi jirani kuwa ni amani na usalama wake na kuongeza kuwa, hadi sasa amefanya mazungumzo va vikao zaidi ya 50 na viongozi wa nchi mbalimbali na kwamba vikao na mazungumzo hayo yamejikita katika suala la kuwepo ushirikiano.
-
Shahram: Iran iko mstari wa mbele kustawisha amani, urafiki kimataifa
Sep 04, 2021 22:15Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeri Shahram Irani anasema Jamhuri ya Kiislamu iko mstari wa mbele katika kampeni ya kuanzisha na kukuza amani na urafiki wa kimataifa.
-
Rais wa Iran aomboleza kifo cha Ayatullah Saeed Al Hakim
Sep 04, 2021 22:04Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuaga dunia Ayatullahil Udhma Sayyid Mohammad Saeed Tabatabai Hakim wa Iraq.
-
Khatibzadeh: Viongozi wa sasa wa Marekani wanafuata njia iliyofeli ya serikali iliyopita
Sep 04, 2021 03:30Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema viongozi wa sasa wa Marekani wanafuata njia ileile iliyofeli na kugonga mwamba ya serikali iliyopita ya nchi hiyo.
-
Amir-Abdollahian: Iran iko tayari kuiuzia Lebanon mafuta zaidi
Sep 03, 2021 21:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuendelea kuiuzia serikali na wafanyabiashara wa Lebanon mafuta.
-
Mtazamo wa serikali mpya ya Iran kuhusu kuhuishwa mazungumzo ya nyuklia
Sep 03, 2021 21:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa na Austria kuhusu sera za kigeni zenye mlingano, kuratibu uhusiano wa Iran na Umoja wa Ulaya na mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Ershadi: Iran ni mhanga mkubwa wa silaha za kemikali duniani
Sep 03, 2021 02:05Naibu mwakilishi wa kudumu wa Iran katika umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mhanga mkubwa wa silaha za kemikali inatoa wito wa kutekelezwa kikamilifu, kwa njia athirifu na bila ya ubaguzi mkataba wa kuzuia silaha za kemikali.